Loading...

MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

Loading...
MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.
link : MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

soma pia


MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

Na John Mapepele, Mara.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata samaki na mazao yake vilivyofungwa katika Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua kabla ya kufikia mwezi Machi mwaka wizarani kwake.

Alivitaja viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited vilivyopo Mwanza na Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited katika mkoa wa Mara.Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba ulinzi wa raslimali hizi ni wa kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha hapa nchini” alisisitiza Mpina 

Waziri Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele) 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika Wilaya ya Butiama leo. 
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu Kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akisoma majina ya Wavuvi Haramu 



Hivyo makala MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

yaani makala yote MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mpina-aagiza-viwanda-vya-samaki-kanda.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU."

Post a Comment

Loading...