Loading...

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU

Loading...
SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU
link : SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU

soma pia


SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU


SERIKALI
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli imeapa 
kutowafumbia macho viongozi au watu wanaojihusisha na shughuli za uvuvi 
wa kutumia zana haramu zilizopigwa marufuku.

Kauli hiyo imetolewa
na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipokuwa akiteketeza
zana za uvuvvi haramu zilizomakatwa hivi karibuni katika Wilaya za 
Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.

Amesema kuwa hakuna atakayesalimika katika sakata hilo endapo tu akibainika kutumia zana haramu za uvuvi.Ameongeza
kuwa Serikali ina dhamira kubwa na wavuvi katka ufanyaji wa shughuli 
zao na ndio maana imeamua kupiga marufuku zana zote haramu kwa lengo la 
kusaidia kizazi kijacho ili nacho kije kinufaike na raslimali za Taifa 
hili.

,"Hivyo idara ya uvuvi kamwe hautomfumbia macho kiongozi 
yeyote yule ambaye anajishughulisha na biashara hiyo kwa kigezo cha kuwa
yeye ni kiongozi.“Kwa yule atakayebainika kuwa ni kiongozi au mtu 
mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu ambao Serikali inatumia 
fedha nyingi kukabiliana nao basi cha mtema kunde atakiona juu yake 
kwani zana zake zitachomwa,faini na yeye kuchukuliwa hatua za kisheria,”
amesema. 

Aidha Ulega amewataka wavuvi kuendelea kusalimisha 
zana haramu kabla ya kukumbwa na dhahma kubwa itakayowapeleka mahali 
pabaya zaidi ya hali ya sasa jinsi ilivyo.Pia amewahakikishia 
upatikanaji wa zana zinazohitajika mapema kwani tayari wamesha anza 
kupokea maombi mengi ya mashirika yanayohitaji kusambaza zana halali 
katika nchi yetu kwa madhumuni ya kuokoa rasilimali za majini zilizokuwa
zikipatwa na shinda nyingi kutoka kwa wavuvui wasiokuwa waaminifu.

Kwa
upande wake Msimamizi wa Kamati Maalumu ya kuthibiti na kupambana na 
uvuvi haramu Kanda ya Simiyu na Mwanza, Nchama Marwa amemuhakikishia 
Naibu Waziri kuwa hakuna uonevu wa aina yeyote ile unaofanywa na kikosi 
hicho kuhusu kuwawajibisha wale wanaoendelea na shughuli hiyo kwa 
kujifisha .Ameongeza kuwa kuna wavuvi ambao wanasalimisha na wengine 
bado wanaendelea kuvua kwa kujifisha laniki ni lazima tu watawakamata na
sheria ya uvuvi itafuata mkondo wake bila kinyongo wala uonevu wa aina 
yeyote ile.

Aidha kiongozi huyo wa kikosi maalumu aliwasilisha 
taarifa kuhusu utekelezaji wa kazi zao kwa Naibu Waziri na kumweleza 
kuwa kuwa mpaka sasa wamekamata nyavu haramu za makila 33121,nyavu za 
dagaa175,makokoro ya sangara119.Pia nyavu za timba 3,sangara wabichi 
kilo 1071,sangara kayabo3463, watu hao waliokamatwa na kikosi kazi 
wametozwa faini kulingana na kile walichokamatwa nacho na kufikia kiasi 
cha Sh.milioni 767.

Naye Boniface Mkama Mkazi wa Nyamikoma 
wilayani Busega ameipongeza Serikali kwa kuwasaidia na vitendo vya 
kinyama vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wavuvi wenzao.Hivyo ameiomba kuwawaishia tu zana sahihi ili waendelea na shughuli zao za kila siku za uvuvi.


Hivyo makala SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU

yaani makala yote SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/serikali-kutowafumbia-macho.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU"

Post a Comment

Loading...