Loading...

VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA

Loading...
VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA
link : VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA

soma pia


VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA

Na Karama Kenyunko-Globu ya jamii.

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi wa Serikali na wanasiasa wenye mamlaka ya kikatiba na kisheria kutoingilia muhimili wa Mahakama badala yake waongoze katika misingi yao.

Amesema kumekuwa na uvunjwaji na kudharauliwa kwa amri zinazotolewa na Mahakama  ambayo imepewa mamlaka ya kikatiba ya kutoa haki.Jaji Profesa Juma amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ya wiki ya sheria itakayoanza Januari 27 mwaka huu. 

Amesema,  suala la utoaji haki ni la Mahakama pekee na kwamba viongozi hao wajiepushe kuingilia maeneo yaliyondani ya haki na hadhi ya mamlaka ya kikatiba ya Mahakama.

Amefafanua ibara ya 107A (1) ya Katiba inayozungumzia mamlaka ya utoaji haki inakumbusha kwamba ‘Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar,hivyo hakuna chombo cha Serikali wala Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.

 Amesema kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapa taarifa kuhusiana na uvunjwaji wa haki ya kikatiba na kwamba mahakimu ndio wenye hadhi ya kulinda haki hiyo.Amesisitiza kuwa amri zinazotolewa na mahakimu zinavunjwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, hivyo ni wakati wa kuwa kama Bunge ambalo watu wake wanapokiuka taratibu wanachukuliwa hatua.

Amesema, mtu yeyote akajivika nguvu za Mahakama atachukuliwa hatua kwani watakuwa wakali kwa watu wataoingia katika anga za mahakama, na kuomba Katiba ifuatwe na sheria ipewe nguvu na wale wote waliopewa mamlaka wabaki katika maeneo yao, 

Akizungumzia wiki ya sheria, Jaji Profesa Juma ameeleza kuwa maadhimisho ya wiki ya Sheria yataanza Januari 27 hadi 31, mwaka huu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atayazindua  katika viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka  yatakapohitimishwa Februari Mosi ambayo itakuwa ni siku ya Sheria.

Amesema, katika wiki hiyo, kutakuwa na utoaji wa elimu ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi watakaoshiriki  maadhimisho hayo  kwa kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama na wadau wa sekta ya sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31,Januari 2018.  Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Hussein Kattanga.


Hivyo makala VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA

yaani makala yote VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/viongozi-wa-serikali-wanasiasa-acheni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA"

Post a Comment

Loading...