Loading...
title : AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE
link : AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE
AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE
Na Agness Francis, Globu ya jamii
KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania, imeendelea kutoa zawadi kwa wateja wake kupitia promosheni ya SMATIKA yatosha na Intanenti Bando inayoendelea kufanyika nchini.
Ambapo wateja wa Airtel hujishindia GB na zawadi zingine ikiwa ni simu za mkononi aina ya Smartphone na Modern ya Maajabu. Pia leo kampuni hiyo imemkabidhi mshindi wa simu aina ya Smartphone Mussa Ngai ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando baada ya makabidhiano hayo akiwa kwenye duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dar es salaam kuwa sasa wamefikia droo ya 10 kufanyika katika promosheni hiyo ambayo bado inaendelea kwa siku 30 zaidi.
"Tumetimiza wateja 21,000 waliojishindia GB za bure na 30 waliojishindia simu na Modern ya maajabu kwa wateja wetu endeleeni kununua bando ili muweze kujishindia zawadi mbalimbali kutoka kwetu,"amesema Mmbando.
Aidha Msimamizi wa duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dorice Opiyo amewakaribisha wateja ambao ni wakazi wa maeneo hayo kupata huduma za kurejesha laini na kujipatia salio kwa wale wanatoa huduma za mawaka
Mshindi wa simu aina ya Smartphone, Mussa Ngai mkazi ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, akizungumzia kushinda promosheni hiyo amesema amefurahi kushinda kwani hakutegemea na alikuwa akinunua bando na kujiunga mpaka siku alipopigiwa simu kutoka Airtel ya kuambiwa ameshinda simu aina ya Smartphone.
Mshindi wa Smartphone Mussa Ngai akikabidhiwa zawadi leo na Dorice Opiyo Msimamizi wa Brunch ya Airtel Money Ya Ukonga Mzambarauni Jijini Dar es salaam.Mshindi wa simu ya Smartphone Mussa Ngai akikagua simu yake mara baada ya zoezi la makabidhiano kumalizika leo katika tawi la Airtel Money Ukonga Mzambarauni Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa simu ya Smartphone Mussa Ngai akipiga picha na wasimamizi wa Brunch ya Airtel money Ukonga Mzambarauni Jijini Dar es Salaam mara baada ga kukagua zawadi yake aliyoshinda kupitia promosheni ya SMATIKA na yatosha Intanenti bando.
Hivyo makala AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE
yaani makala yote AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/airtel-yaendelea-kutoa-zawadi-kwa.html
0 Response to "AIRTEL YAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE"
Post a Comment