Loading...
title : WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI
link : WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI
WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
WAFUASI watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
leo, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa
tuhuma za kufanya mkusanyiko isivyo halali.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amewataja washtakiwa hao watatu
kuwa ni, Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi ambao wanadaiwa
kupigwa risasi na jeshi la polisi waliofikishwa kizimbani kwa Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wakiwa na majeraha katika sehemu za miguu na mapaja yakiwa yamefungwa bandeji.
Washitakiwa hao Machi 8, mwaka huu wataunganishwa na wenzao
28, wanaodaiwa kutenda kosa pamoja.Kwa pamoja wanadaiwa,
Februari 16, mwaka huu, huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni
lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko
usio wa halali kinyume cha sheria kwa nia ya kufanya uvunjifu wa
amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.
Wametajwa baadhi ya washitakiwa hao 28 ni Thabita Mkude, Haji
Lukwambe, Emmanuel Kimoi,Mohammed Juma, Hussein Mrombo,
Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein
Nguli na Edna Kimoro.
Wengine ni Jonathan Lema,Salha Ngondo, Ramadhan Mombo,
Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda,Omary Hamad, Fatima
Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa,Dickson Kerefu,
Raphael Mwaipopo, At human Mkawa, Mussa Kusigila, OMARY Danga,
Jackson Masilingi,Asha Kileta na Ally Rajabu.
Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana.
Baada ya kuachiwa kwa washtakiwa hao watatu ndugu zao waliwakumbatia na kuangua vilio mahakamani hapo.Kwa upande wake Wakili wa washtakiwa Alex Masaba alisema wamemaliza suala la msingi la wafuasi hao waliokamatwa Mkwajuni,ambao mwanzo hawakuletwa mahakamani lakini wenzao 28 waliletwa mahakamani na walipata dhamana
Alisema walifuatilia katika vituo vya polisi kwa siku 12 ambapo
walishindwana na polisi ambapo Februari, 26,mwaka 2018
walipeleka maombi Mahakama Kuu na juzi walipangiwa tarehe ya
kusikilizwa maombi yao ambayo ni jana.

Hivyo makala WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI
yaani makala yote WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wafuasi-watatu-chadema-wafikishwa.html
0 Response to "WAFUASI WATATU CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI"
Post a Comment