Loading...
title : KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO
link : KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO
KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO
Kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya malipo, imetangaza rasmi ushirikiano wa kimkakati kati yao na Maxcom Afrika ambayo itawawezesha wauzaji zaidi ya 30,000 kupokea malipo ya Visa kwa kutumia simu ya mkononi pamoja na mawakala 20,000 ambao watawezeshwa kupokea amana na kutoa malipo na kuunganisha watanzania na mfumo wa kimataifa wa malipo.
Kampuni ya Visa imejitolea kuleta njia rahisi zaidi, za kuaminika na salama za kufanya malipo duniani kote. Sasa, pamoja na malipo kwa kadi za plastiki, wateja wanaweza kutumia simu zao kufanya malipo kwa Visa.
Visa kwenye simu itawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali au kutuma pesa kwa familia na marafiki, bila kukatwa malipo.
Huduma hii ambayo inatolewa kupita akaunti ya benki huunganisha akaunti ya mteja ya benki na hudumza za benki za simu bila na kuwezesha mteja kufanya malipo ya ndani nan nje ya nchi kwa kutumia huduma ya Visa kwa simu.
Pia huduma hiyo itawezesha huduma za kuweka na kutoa pesa kwa kutoka kwa mawakala wa benki maalumu na ushirikiano huo na Maxcom Afrika utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kulipa kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji wapya zaidi ya 30,000.
"Ushirikiano huu unasisitiza jinsi Visa wamejitolea kuhakikisha na kupanua wigo wa malipo kwa malipo ya simu duniani kote, "alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Sunny Walia.
Maxcom Afrika inatoa njia rahisi, salama na ya kuaminika ya kufanya malipo kwa watu binafsi na biashara nchini Tanzania.
Maxcom Afrika inawezesha malipo kwenye mtandao na moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.
Wamejenga vipengele vya usalama kulinda wanunuzi na wauzaji wote kwa kuhakikisha taarifa za shughuli zinafichwa kwa kutumia viwango vya benki huku wakikutuma taarifa ya malipo kwa akaunti za benki. Maxcom Afrika inatoa malipo ya hapopapo, huduma za mtandao na huduma kwa njia ya simu iliyounganishwa na terminal ya usindikaji kadi.
Viongozi wa Maxcom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Kampuni ya Visa baada ya kuingia makubaliano ya kimkakati kwa kupokea malipo na amana kupitia mfumo wa kimataifa wa malipo
Hivyo makala KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO
yaani makala yote KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/kampuni-ya-kimataifa-visa-on-mobile.html
0 Response to "KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO"
Post a Comment