Loading...
title : AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI
link : AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI
AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI
MKAZI wa kijiji cha Mpanji kata ya Mbati wilayani Tunduru Awetu Mussa(52) amefariki Dunia baada ya kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya mwili wake na kundi kubwa la Tembo.
Tukio hilo lilitokea tarehe 22 Mwezi huu, ambapo marehemu alipatwa na mkasa huo wakati akielekea shambani na mumewe Ahmad Kisanje ambapo wakiwa njiani majira ya asubuhi walikutana na kundi hilo la Tembo ambao walipumzika chini ya mti na mara baada ya kuwaona walibadili mwelekeo wa safari yao na kuanza kuwafuata.
Kwa Mujibu wa mume wa marehemu Ahmadi Kisanje ni kwamba, licha ya marehemu kujitahidi kukimbia kwa lengo la kuokoa maisha yake lakini alizidiwa mbio na Tembo hao ambao walimuangusha chini na kumkanyaga ambapo Awetu alifariki Dunia papo hapo.
Kisanje alisema,yeye aliweza kunusurika kutokana na kujificha nyuma ya kisiki kikubwa huku akishuhudia mke wake akipoteza Dunia kwa kukanyagwa maeneo mbalimbali ya mwili.
Tembo hao ambao wanatembea makundi makubwa kuanzia 20 na kuendelea, wanatoka katika Hifadhi ya Selou na mapori yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa misitu wamekuwa wakiharibu mazao mashambani na kuleta tahuruki kubwa kwa wananchi hivyo kusababisha hata kushindwa kwenda katika shughuli zao mashambani.
Ameiomba Serikali kupeleka Askari wa Wanyama poli wengi katika kijiji hicho ili kurudisha hali ya amani na utulivu kwani kama Tembo wataachwa bila kudhibitiwa kuna hatari ya wananchi kushindwa kwenda katika shughuli za uzalishaji mali.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye alifika nyumbani kwa Marehemu kwa lengo la kuipa pole familia ya iliyompoteza mpendwa wao alisema, Serikali imesikitishwa na tukio hilo na imeshapeleka Askari kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama poli(TAWA)kanda ya Songea ambao wameanza kazi ya kufukuza tembo kurudi katika makazi yao ya kawaida.
Homera ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Tunduru amewataka Wananchi wa kijiji hicho na maeneo mengine kuchukua taadhari pindi wanapokwenda mashambani na kuaghailisha safari zao pindi wanapoona dalili za uwepo wa wanyama hao.
Alisema, serikali inathamini sana maisha ya wananchi,lakini ni lazima nao wawe na tabia ya kuchukua taadhari ikiwemo kutolima jirani na maeneo ambayo yamehifadhiwa kwa ajili ya wanyama.
Akiongea katika mkutano na wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa wilaya alisema, serikali haitalipa fidia wala kutoa kifuta jasho kwa mtu yoyote atakayejeruhiwa na wanyama ambaye anafanya shughuli zake katika maeneo yasioruhusiwa kufanya shughuli za kibinadamu.
Kwa upande wake, mkuu wa kikosi cha Mamlaka ya usimamizi Wanyamapoli kanda ya kusini Ruben Joseph amewataka wananchi kuwa makini pindi wanapokwenda mashambani na ikiwezekana kusubiri kwa muda wakati huu ambao wanaendelea kurudisha makundi hayo ya Tembo katika hifadhi.
Wakati huo huo kundi kubwa la Tembo linakadiliwa kufikia 30 wamevamia shamba lenye ukubwa wa ekari tano la mtendaji wa kijiji cha Mbesa wilaya ya Tunduru Rasso Kundeka na kuharibu na kula matikiti zaidi ya elfu tano.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kulia akimpa pole Mzee wa kijiji cha Mpanji kata ya Mbati Ahmed Kisanje baada kufiwa na mkewe Awetu Musa kutokana na kushambuliwa na kuawa na Tembo alipokuwa njiani kuelekea shambani .
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori kanda ya Kusini Ruben Joseph akiongea na wananchi wa kijiji cha Mpanji wilaya ya Tunduru baada ya kutokea kifo cha mkazi wa kijiji hicho baada ya kushambuliwa na Tembo wakati akienda shambani,katikati Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mpanji wilaya ya Tuunduru wakinyanyua mikono kama ishara ya kukubali kuanza ujenzi wa zahanati baada ya wananchi hao kukosa huduma za Afya kwa miaka mingi ambapo Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera(hayupo pichani) kuchangia mifuko 100 ya saruji na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori kanda ya Kusini nayo kutoa mifuko 10.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera wa pili kushoto akiangali mabaki ya Tikiti baada ya kundi kubwa la Tembo kuvamia na kufanya uharibifu wa mazao katika shamba la mtendaji wa kata ya Mbesa Rasso Kudeka.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akikagua shamba la Afisa Mtendaji wa kata ya Mbesa Rasso Kundeka ambalo kundi la Tembo lilivamia na kufanya uharibu mkubwa wa mazao ikiwemo Matikiti,viazi na mbaazi.
Hivyo makala AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI
yaani makala yote AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/auawa-na-tembo-akiwa-njiani-kwenda.html
0 Response to "AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI"
Post a Comment