Loading...

TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China

Loading...
TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China
link : TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China

soma pia


TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama za safari na pia kuchochea utalii.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.

akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa ndani kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio makubwa.

Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea idadi kubwa ya watalii kutoka China. Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya utalii.


Hivyo makala TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China

yaani makala yote TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/ttb-yapigia-chapuo-safari-za-ndege-moja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China"

Post a Comment

Loading...