Loading...
title : ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY
link : ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY
ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY
Na: Patrick John
Jumapili ya leo waingereza wanaiita super sunday kwani ina mtiririko wa mechi nyingi kubwa kuanzia hapa nchini hadi huko ulaya. Huko Italia kutakuwa na Rome derby itakayozikutanisha As Roma dhidi ya Lazio mchezo utakaopigwa katika dimba la stadio olimpico bila kusahau mechi itakayofunga siku huko huko Italia baina ya inter milan dhidi ya ssc napoli. Nchini Uingereza ligi kuu itaendelea na kubwa ni mchezo wa watani wa jadi kama tunavyowaita hapa nyumbani au North London derby kama waingereza wanavyoitamka mchezo utakao zikutanisha Tottenham Hotspurs wakiwakaribisha mahasimu wao Arsenal katika dimba la white Hart Lane mchezo utakaochezwa majira ya saa kumi na mbili na nusu kwa saa za afrika ya mashariki.
Timu:
Arsenal wanakwenda kwenye mchezo wakiendelea kukosa huduma ya beki wao Shkrodani mustafi na kuna hatihati ya kucheza kwa nahodha wao msaidizi Laurent Koscienly ambae ni mmoja ya wachezaji muhimu kwa timu hiyo. Bado ndoto zao kutinga top four hazijakatika ila matumaini yanaweza kuondolewa na kipigo kutoka kwa spurs.
Spurs wao wanaingia uwanjani wakiwa na morali lakini wakijihami mno na kuweka umakini kwani bado milango ya ubingwa haijafungwa bado, bado kuna imani kuwa lolote linaweza kutokea kwa chelsea hivyo kuteleza kwao kutarahisisha ufungaji wa mlango wa ubingwa wa ligi kuu uingereza .
Rekodi
Kwa rekodi za mchezo mitano ya ligi kuu uingereza baina ya timu hizi inaonesha Tottenham akiwa ameshinda mchezo mmoja na kupata sare kwa michezo mingine Minne, ikiwa ni rekodi kubwa kwa spurs dhidi ya Arsenal. Mchezaji wa kulindwa zaidi ni Harry kane kwani amekuwa na muendelezo mzuri katika ligi dhidi ya Arsenal na amefanikiwa kuwafunga mabao 5 na manne yakiwa ni mfululizo ( consecutive) dhidi ya arsenal ambayo imekuwa na kipindi cha kupanda na kushuka kwa michezo ya hivi karibuni.
Arsenal katika michezo mitano ya karibuni waliyocheza, wamefanikiwa kushinda michezo minne na kufungwa mmoja. Huku Spurs nao katika michezo mitano ya karibuni wamefanikiwa kushinda mechi 4 na kufungwa mechi 1 na Chelsea katika nusu fainali kombe la FA.
Makocha na mifumo:
Mauricio pochetino amekuwa na muendelezo mzuri katika ligi kuu ya uingereza tangu alipoanza kuifundisha southampton na sasa Tottenham amefanikiwa kuwa kocha wa kwanza kucheza michezo mitano ya ligi bila kupoteza baina ya spurs na Arsenal na pia amefanikiwa kuiongoza spurs kushinda michezo minane ya ligi mfululizo toka mwaka1960. Pochetino amekuwa akiutumia sana mfumo wa 4-2-3-1 unaomfanya kuwatumia Wanyama na Dembele katika eneo la kiungo mkabaji. katika mechi za karibuni amekuwa akitumia mfumo wa 3-4-3 kwa ajili ya kushambulia kwa kasi lakini natumaini kumwona akirejea kwenye mfumo wa awali ili kuhakikisha timu inapata balance .
Arsene Wenger amekuwa na wakati mgumu kutokana namatokeo mabovu ya timu yake, katika mchezo huu atakuwa anafikisha mchezo wake wa hamsini dhidi ya spurs akifanikiwa kushinda 22 kutoka sare 20 na amepoteza 7 huku timu yake ikifunga magoli mengi dhidi ya spurs magoli 92 .Mzee huyu wa kifaransa ni muumini wa soka la kuvutia kwa pasi nyingi amekuwa akitumia mfumo 4-2-3-1 mfumo uliokuwa ukimpa matokeo lakini mambo yalipo badilika ameanza kuutumia mfumo 3-4-3 mfumo ambao umempa matokeo mazuri katika mechi tatu za hivi karibuni nategemea kumuona akiendelea kuutumia mfumo wa beki wa tatu kuilinda ngome inayoongozwa na mlinda mlango mkongwe Petr Cech .
Kama ilivyo michezo iliyopita ya North London derby mchezo huu utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi na vile spurs wanataka kumaliza juu ya washika bunduki hawa wa London, natabiri matokeo ni 3-1.
Hivyo makala ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY
yaani makala yote ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/arsenal-na-spurs-leo-kutafuta-mbabe-wa.html
0 Response to "ARSENAL NA SPURS LEO KUTAFUTA MBABE WA NORTH LONDON DERBY"
Post a Comment