Loading...

Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.

Loading...
Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.
link : Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.

soma pia


Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.







Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wafanyakazi wanapaswa kujitahidi kutekeleza majukumu yao ya Utumishi wa Umma kwa kufanya kazi kizalendo na  ushirikiano uliotukuka ili  kujijengea mazingira bora ya hatma yao ya baadae.

Alisema tabia hiyo njema itawapa  heshima kubwa katika Jamii kiasi wamba wamalizapo muda wao wa Utumishi watajikuta wakiacha athari inayoendelea kukumbukwa kwa wema na watumishi wenzao waliowaacha.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuwapongeza na kuwaaga Wafanyakazi 13 waliostaafu kati ya Mwaka 2015/2016 na 2016/2017 wa Idara tofauti zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema haipendezi na ni hulka mbaya inayowakumba baadhi ya Watumishi wa Umma hawa wale wenye mardaraka pale wanapofikia muda wao wa kustaafu na walio nyuma  yao wakasherehekea kwa Pilau kutokana na vitendo  vyao vilivyokosa imani kwa kutowatendea haki.

Balozi Seif aliwapongeza Wafanyakazi wote waliostafu  kwa kumaliza Utumishi wao katika njia ya salama na afya njema iliyopatikana kwa wao kuzingatia na kufuata mashauri ya Kitaalamu ya Afya katika mfumo wa kufanya mazoezi baada ya muda wa kazi.

Aliwataka wafanyakazi wanaofikia umri wa kustaafu kuachana na tabia ya kujenga hofu kipindi wanachokaribia kumaliza muda wao wa Utumishi kwani kinaweza kuwasababishia msongo wa mawazo yanayoishia kupata maradhi.

Balozi Seif alitanabahisha wazi kwamba kustaafu sio mwisho wa maisha lakini kinachotakiwa  kwa wastaafu hao ni kujipanga vyema ili kukabiliana na mabadiliko ya maisha mapywa wanayoyaingia.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wafanyakazi wapya na wale wanaoendelea na utumishi wao kutumia maarifa, uzoefu, ujuzi na hata mbinu zilizokuwa zikitumiwa na watangulizi wao waliostaafu ili kupata ufanisi mzuri kwa Wizara na Taifa kwa ujumla.

Mapema akitoa Taarifa fupi ya wafanyakazi hao wastaafu, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi Halima Ramadhan Toufiq alisema Utumishi wa Wafanyakazi hao wastaafu katika Taasisi za Umma umesaidia kizazi kipya katika kuendeleza gurudumu waliloliacha.

Bibi Halima alisema licha ya wastaafu hao kuwa na uwezo kamili wa kuwajibika zaidi lakini Kifungu cha 68 {1} cha Utumishi wa Umma kimeweka bayana kuhusu kumaliza kwa Mkataba wa ajira.

Mkurugenzi huyo wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wastaafu hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wapya ili kuwapa maarifa yatakayowasaidia kumudu vyema kutekeleza kazi zao.

Bibi Halima aliwataja Wafanyakazi hao 13 wastaafu kuwa ni pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Waziri Kiongozi na Ndugu Abdulla Ali Abdulla Kitole aliyekuwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Wengine aliowataja ni Nd. Khatib Said Khatib aliyekuwa Mkurugenzi Uratibu, Bibi Shinuna Idara ya Faradha, Nd. Makame Mussa, Nd. Hassan Mohamed  Hassan ,  Nd. Tajo Hussein Mawele, Bibi Amina Hussein Haji, Maabad Mlekwa Maabad, Siende Khatib Khamis, Mafunda Khamis Hamad,  Kiboga Suleiman na Aziza Khalef Mohamed.

Wastaafu hao pamoja na mambo mengine walikabidhiwa vyetu maalum, zawadi mbali mbali kulingana na kada zao pamoja na fedha taslim kama ni ukumbusho kwao kutokana na utumishi wao mzuri  uliotukuka.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wastaafu  wenzake 13 Mstaafu nambari moja katika kundi hilo Mama Asha Suleiman Iddi alikiasa Kikazi kipya kinachoingia katika ajira mpya iwe ya Umma na hata ya Sekta binafsi kuacha tamaa ya kutaka kujilimbikizia mali na utajiri ndani ya kipindi kifupi cha ajira zao.

Mama Asha alisema kitendo hicho ambacho hushabikiwa na baadhi ya watu mitaani kwa kuonekana mjanja na mwenye maarifa mbali ya kuhatarisha ajira zao laikini pia kinakwenda kinyume na kanuni, maadili na heshima ya Kazi.

Akizungumzia suala na viinua mgongo vya watumishi wastaafu Mama Asha aliziomba Taasisi zinazosimamia masuala hayo kufanya juhudi za ziada katika kuona haki za wastaafu hao zinapatikana kwa wakati muwafaka bila ya kuleta kughdha yoyote.

Alisema zipo dalili zinazoonyesha kuwatia hofu baadhi ya watumishi wastaafu kutokana na kucheleweshewa   masurufu yao ambayo tayari wameshalenga kuwaendelesha katika muda wao wa kumalizia maisha.


Hivyo makala Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.

yaani makala yote Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/balozin-seif-awataka-wafanyakazi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozin Seif Awataka Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi."

Post a Comment

Loading...