Loading...
title : Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo
link : Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo
Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo
Na Salmin Juma Pemba.
WAKAAZI wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wako hatarini kupata ugonjwa wa goita pamoja na matatizo ya kuzaa watoto wenye udumavu wa akili na kuharibu mimba kwa akinamama baada ya kubainika kuwa chumvi yenye madini joto haitumiki ipasavyo katika Wilaya ahiyo.
Mkuu wa kitengo cha Lishe cha Wizara ya Afya Pemba Raya Mkoko amesema kuwa utafiti uliofanywa katika familia 2,685 ni familia 345 sawa na asilimia kumi na tatu (13%) ambazo zimebainika kuwa zinatumia chumvi zenye madini joto.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake Wete , Raya amesema utafiti huo umefanywa na maafisa Lishe ambao walipita katika Skuli na kuwataka wanafunzi kila mmoja kuchukua chumvi wanayotumia nyumbani na kubainika familia 2,340 zinatumia chumvi isiyo na madini joto.
Raya Mkoko ameitaka jamii hususani ya Wilaya ya Micheweni kuifanyia uchunguzi wa chumvi ambazo wananunua kwa kutumia njia asili kuiangalia ili kujiridhisha kama kuna madini joto kabla ya kuinunua na kutumia .
Afisa Mkaguzi wa bodi ya Chakula , Dawa na Vipodozi Pemba Juma Seif Khamis amesema bodi imejipanga kutumia sheria kwa mkulima na muuzaji ambaye atabainika kusambaza na kuuza chumvi isiyokuwa na madini joto .
Amesema awali bodi , kitengo cha Lishe pamoja na wazalishaji wa chumvi Pemba walikubaliana kuwa , kila upande uchukuwe hatua za utoaji wa elimu kwa wananchi huku akisema hatua za kihseria zitachukuliwa kwa atakaye kaidi .
Hivyo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa taasisi husika baada ya kubaini kwamba kuna chumvi inauzwa na ambayo haina madini joto ili muhusika aweze kuchukuliwa hatua kisheria ikiwa ni pamoja na kuiangamiza chumvi hiyo .
Hivyo makala Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo
yaani makala yote Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/chumi-ya-madini-joto-haitumiki-ipasavyo.html
0 Response to "Chumi ya Madini Joto Haitumiki Ipasavyo"
Post a Comment