Loading...

JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE

Loading...
JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE
link : JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE

soma pia


JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE


Anthony Ishengoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya vituo 9 katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais,Kamishna wa Ustawi wa jamii Bw. Rabikira Mushi amesema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

Akifafanua Mushi amesema Mikoa ingine iliyofaidika na zawadi hizo ni Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga, Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida, Mwanza, na Pwani.

Aidha vitu vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao ya Watoto Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha,Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.

Viuo vingine ni Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund, Temeke.Makao ya Watoto Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization),Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge Kigamboni.

Kwa upande wa Zanzibar Bw. Mushi alitaja Vituo vilivyonufaika na zawadi hizo,Kituo cha Watoto Istima - Chakechake, PembaMakazi ya Wazee Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

Aidha kwa Mikoa ya Tanzania Bara jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya Mhe. Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro,Mahabusu ya Watoto Mbeya,Mahabusu ya Watoto Arusha,Mahabusu ya Watoto Tanga,Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzage Tanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.

Utoaji wa zawadi umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Waheshimiwa Marais tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa sista Stella Selugenge wa Kituo cha Kulelea watoto cha Msimbazi Center leo Jijini Dar es Salaam. 
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
. Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam. 
. Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Veronika Msanjila wa Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge leo Jijini Dar es Salaam.

(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).


Hivyo makala JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE

yaani makala yote JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/jpm-atoa-zawadi-za-pasaka-vituo-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JPM ATOA ZAWADI ZA PASAKA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA MAKAO YA WAZEE"

Post a Comment

Loading...