Loading...
title : Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo
link : Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo
Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo
Grace Gurisha
KESI ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili vigogo wawili wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha ushahidi, baada ya washitakiwa kusomewa maelezo yao ya awali.
Kesi hiyo namba 102 ya 2017 itasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, ambapo upande wa Jamhuri utawakilishwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru.)
Vigogo hao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Cosmas Mwaifwani na Kaimu Meneja Ununuzi, Frederick Nicolaus, ambao waliposomewa maelezo hayo walikubali majina yao na vyeo vyao, lakini wakakana tuhuma zinazowakabili.
Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Machi mosi na 19, 2013 wakiwa makao makuu ya MSD Temeke, Dar es Salaam, kwa nafasi zao walitumia madaraka vibaya kuandaa, kusaini mkataba namba moja wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/1011/60 wa Machi mosi, 2013.
Pia wanadaiwa kuwa waliandaa waraka wa mwito namba 2 wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/2011/60 wa Machi 19, 2013 na kuisababishia kampuni ya H.H. Hillal & Company Limited kupata manufaa ya Sh 482,266,000.
Baada ya kusomewa mashitaka, walikana na kuwa nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Hivyo makala Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo
yaani makala yote Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/kesi-ya-vigogo-msd-kusikilizwa-leo.html
0 Response to "Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo"
Post a Comment