Loading...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar.

Loading...
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar.
link : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar.

soma pia


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar.










Na. Othman Khamis OMPR. 
Matukio ya uvunjifu wa sheria za usalama Barabarani bado yanaendelea kuoteza nguvu kazi  ya Taifa wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.

Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu  ya Bara bara na vifaa vyengine.

Balozi Seif alisema ajali za bara barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii  sheria na taratibu zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.

Alisema baadhi ya madereva hao wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi bila ya kujali watumiaji wengine  mbali mbali kama watoto ambao nao wana haki ya matumizi ya bara  bara hizo.

Balozi Seif  alionyesha masikitiko yake kutokana na baadhi ya madereva husababisha ajali za kizembe kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama Bara barani  hapa Zanzibar ni wa busara  na kuwa wakati muwafaka ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali za bara barani.

Akizungumzia upande wa gari za Dala dala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kipo kilio kikubwa cha abiria kutokana na vitendo vya madereva na makonda  vya kutowafikisha katika vituo vyao walivyopangiwa.

Alisema mambo hayo yanawasumbua abiria hasa wale wenye mahitaji maalum walemavu ambayo yanakwenda kinyume na sheria za usalama bara barani pamoja na kanuni zake.

Balozi Seif alieleza kwa kutumia utaratibu wa Mabalozi wa Usalama Bara barani wakati umefika wa kukabiliana na matukio  kwa kuwapa Taarifa kwa wakati na kuchukuliwa hatua dhidi ya watu wote wanaohusika kuvunja sheria za Nchi.

Jeshi la Polisi usalama Bara barani pamoja na mamlaka nyengine ni vyema likashirikiana kwa karibu na Mabalozi wa Usalama Bara barani kwa kusimamia vyema dhana hii kwa kutumia mikakati tofauti itakayowanasa wapinda sheria za usalama bara barani.

Alisema kupaza sauti, kukemea pamoja na kuchukuwa hatua nyengine kwa wale madereva watukutu kutasaidia kuondoa udumbufu na kero zinazotokana na tabia hiyo mbaya ndani ya Jamii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilinasihi jeshi la Polisi kujenga utamaduni wa  kuficha siri kwani ni dhambi kubwa iwapo taarifa za uvunjaji wa sheria bara barani zinazotolewa na Mabalozi  kwa jeshi kutolewa kwa wavunja wa sheria  hizo.

Balozi Seif alifafanua kwamba huo ni usaliti wa wazi na kamwe hautokubalika kwa sababu ni adui wa maendeleo.

Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Justafa Mussa  alisema Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa yanayotokana na bara bara.

Nd. Mustafa alisema dhana hiyo ya Mabalozi wa usalama bara barani inafaa kuungwa mkono ya washirika  mbali mbali  huku wakielewa kwamba jukumu la kulinda usalama wa raia linamuhusu na kumgusa kikla mwana Jamii.

Alisema wanajumiya hao tayari wameshaanza kutoka mafunzo kwa wanafunzi katika maskuli mbali mbali nchini sambamba na kuwataka wana jamii kutowaonea haya madereva na makonda wajeuri.

Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi { ACP } Mkadam  Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea  Bara barani kutokana na vitendo visivyotii usalama bara barani.

ACP Mkadam alisema kikosi cha usalama Bara bara kimekuwa kikibuni mbinu mbali mbali za kusimamia usalama sambamba na kupunguza ajali kwa kiwqango kikubwa kadri inavyowezekana.

Alisema ajali za bara barani zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya watu 147 wakati mwaka 2017 uliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.

Uzinduzi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Zanzibar  ulioambatana na michezo ya kuigiza yenye mnasaba na tukio hilo umeshuhudiwa na wanamtandao wa Mabalozi wa usalama Bara barani kutoka Tanzania Bara wakiongozwa na Naibu Kamishna wa Usalama Bara barani Tanzania ACP Mohamed Mhina.


Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar.

yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_19.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aindua Mabalozi wa Usalama wa Barabarani Zanzibar."

Post a Comment

Loading...