Loading...

MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI

Loading...
MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI
link : MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI

soma pia


MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI

Mwambawahabari

IS 
KITENGO cha usalama barabarani mkoani Pwani, kimeingiza sh.mil.867.810,kutokana na makosa madogo 28,927,yaliyotozwa faini katika kipindi cha Jan-March 2017.

Fedha hiyo imetokana na makosa hayo,ambayo yameongezeka , ukilinganisha na mwaka jana kipindi kama hicho ambapo yalikuwa makosa 24,364.

Aidha pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali ni 4,226 ambapo zimesababisha kukusanya sh.mil.126.780.

Kamanda wa usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango aliyasema hayo,wakati akitoa taarifa ya robo ya mwaka ya makosa ya usalama barabarani.

Alisema Jan -march mwaka 2016 jumla ya makosa madogo 24,364 na mwaka huu yamefikia makosa 28,927 ikiwa ni ongezeko la makosa 4,563.


Alieleza kati ya pikipiki zilizokamatwa  fedha hizo ni ongezeko la sh.mil. 146,610 ukilinganisha na fedha iliyokusanywa Jan -march mwaka jana.

Hata hivyo Issango,alisema kwa kipindi cha miezi mitatu sasa ,idadi ya ajali zote,ajali za vifo na idadi ya watu waliokufa imepungua ukilinganisha na matukio ya ajali za mwaka jana kipindi kama hicho.

Alifafanua,idadi ya watu wanaokufa kwa ajali imepungua kutoka watu 80  katika kipindi cha kuanzia januari hadi machi mwaka jana na kufikia watu 22 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

Alisema katika kipindi hicho idadi ya watu waliojeruhiwa katika ajali hizo ilipungua kutoka 181 hadi kufikia watu 32 .

“Pia kwa kipindi hicho jumla ya ajali zote ilikuwa 162 na kwa mwaka huu wamefanikiwa kupunguza hadi kufikia  ajali 25 sawa na asilimia 84.56”alisema Issango. 

Issango alibainisha kwamba idadi ya ajali za vifo  jan hadi march mwaka 2016 zilikuwa 70 kwasasa ni 20 pungufu ni 50 sawa na asilimia 71.42.

Awali ,mlezi wa kamati ya usalama barabarani mkoani humo ,ambae pia ni kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pamoja na kupungua kwa ajali bado kamati ya usalama barabarani ina kazi yakuendelea kutoa elimu.

“Kamati hii kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani ina kazi kubwa ya kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara wakiwemo wanafunzi “

Kamanda Lyanga alisema endapo watajenga umoja itasaidia kutokomeza suala zima la ajali katika mkoa huo.

“Kila mmoja asimame katika nafasi yake ,kila mtu achukie ajali,toeni elimu kwa wananchi hasa  kwa waendesha boda boda,wanafunzi ambao wamekuwa wakipoteza maisha kwa ajali hizo”, alisema kamanda Lyanga.

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia Paul Teremka(24),na Paul Deogratius (22)walinzi wa Tiblus Michael (40)mkazi wa Mwenge,ili kusaidia uchunguzi dhidi ya tukio la wizi wa ng ‘ombe 40 waliokuwa kwenye zizi huko Kerege kwa Kiwete Bagamoyo.

Kamanda Lyanga, alibainisha katika tukio hilo watu wasiojulikana walivunja zizi na kuiba ng ‘ombe hao wenye thamani ya mil. 40.


Hivyo makala MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI

yaani makala yote MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/makosa-madogo-ya-usalama-barabarani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKOSA MADOGO YA USALAMA BARABARANI YAIINGIZA MAMILIONI PWANI"

Post a Comment

Loading...