Loading...

Mbunge ataka wananchi watunze chakula

Loading...
Mbunge ataka wananchi watunze chakula - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mbunge ataka wananchi watunze chakula, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mbunge ataka wananchi watunze chakula
link : Mbunge ataka wananchi watunze chakula

soma pia


Mbunge ataka wananchi watunze chakula


Suleiman Msuya

Hamidu Bobali
MBUNGE wa Mchinga, Hamidu Bobali, amewasihi wananchi wa jimbo hilo mkoani Lindi kutunza chakula na kujikita katika kilimo cha mazao yanayovumilia ukame, ili kukabiliana na njaa.

Bobali alisema hayo katika mikutano mbalimbali aliyofanya hivi karibuni kwenye jimbo hilo kukagua miradi ya kijamii.

Alisema amelazimika kutoa tahadhari hiyo mapema kwa sababu hali halisi iliyopo nchini inaonesha mwakani njaa itakuwepo.

Mbunge huyo alisema ipo tabia ya wananchi kujihusisha na kilimo na baadae kuuza mazao yote jambo linalopaswa kuangaliwa kwa makini ili wasiathirike baadae.

“Nimelazimika kuwaambia hili hasa nyinyi wananchi wa kitongoji cha Lichinji, mtunze chakula kwani hii mvua mnayoiona hapa huko kwengine haipo na mkumbuke kuwa Serikali haitaleta chakula na mimi sitaweza pia kuleta chakula kwa watu wote,” alisema.

Alisema iwapo kila mwananchi atatunza chakula alichovuna, ni wazi changamoto ya njaa haitakuwepo hivyo wahakikishe   wanauza chakula kidogo.

Mbunge huyo alisisitiza kwa wananchi wa mkoa huo kujikita katika kilimo cha mazao yanayovumilia ukame ikiwemo muhogo, mtama na uwele ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Bobali alisema pamoja na kujikita katika kilimo hicho, ni wakati muafaka kuanza kuandaa mashamba ya korosho, ili msimu ukianza wasitumie gharama kubwa.

“Naomba muyape kipaumbele mazao yanayovumilia ukame kwani kinyume na hivyo tunaweza kuumbuka na msisahau kuanza maandalizi ya mashamba ya korosho mapema,” alisema.

Alisema zao la korosho limekuwa likipanda bei kila siku, hivyo matarajio yake ni kuona wananchi wengi waliosusa mashamba wakirejea na kuyaanda ili wapate mavuno.

Bobali alisema katika hilo hatarajii kuona propaganda zikipewa nafasi, kwani lengo la wabunge wote wa mkoa huo ni kuhakikisha bei ya korosho inazidi kupanda kwa kasi ili wakulima wafaidike.

Akizungumza katika mkutano huo, mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho, Ibrahim Tondoro aliunga mkono hoja ya mbunge na kuwataka wananchi wenzake kujikita katika kilimo chenye tija.

Tondoro alisema ni wazi wananchi wamekuwa wakisahau na kuuza mazao hivyo angalizo la mbunge litaondoa lawama ambazo zimekuwa zikitokea kila mara.


Hivyo makala Mbunge ataka wananchi watunze chakula

yaani makala yote Mbunge ataka wananchi watunze chakula Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mbunge ataka wananchi watunze chakula mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/mbunge-ataka-wananchi-watunze-chakula.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mbunge ataka wananchi watunze chakula"

Post a Comment

Loading...