Loading...
title : Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni
link : Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni
Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni
Waandishi Wetu
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limepiga marufuku wanachama wa CUF, kufanya usafi wa mazingira kwenye ofisi za chama hicho Buguruni.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuomba kufanya usafi kwenye ofisi hiyo Aprili 30.
Alisema Jeshi hilo limetoa zuio kutokana na sababu za kiusalama ambazo zinatokana na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho.
“Tunaomba kila mwanachama wa CUF au mwananchi afanye usafi katika eneo analoishi au ofisini kwake, kwa vile kitendo cha kukusanyika kwa wanachama hao kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema.
Alisema sheria ya Jeshi la Polisi sura namba 322 yenye mapitio ya mwaka 2002, inatoa mamlaka kwa Kamanda kutoa zuio la mkusanyiko huo na kuwataka kutii sheria bila shuruti.
Kamanda Sirro alisema kamwe Polisi haiwezi kuruhusu makundi hayo mawili kukutana eneo moja na tayari wamekutana na viongozi wa chama hicho na kuzungumza.
Katika mazungumzo hayo kwa mujibu wa Sirro, Jeshi la Polisi liliwashauri viongozi hao, Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Seif Sharrif Hamad, mgogoro wao uendelee ndani ya chama na si nje, kwani watasababisha ugomvi na vyombo vya Dola.
Juzi Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF), ilitangaza mchakato wa kusafisha ofisi hiyo kesho.
JUVICUF pia ilitumia fursa ya kukutana na waandishi wa habari, kulaani kitendo cha watu wanaotajwa kuwa kundi la Profesa Lipumba kuvamia mkutano wa waandishi wa habari na kuwajeruhi.
Mwenyekiti wa JUVICUF Taifa, Hamidu Bobali ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, ndiye aliyetoa taarifa juzi akisema wameandaa utaratibu mzuri wa kuwezesha kila kijana mwenye nia kokote aliko Dar es Salaam na maeneo jirani kufika Buguruni.
Bobali alisema lengo na nia ya kwenda Buguruni kwenye Ofisi Kuu za chama hicho, ni kufanya usafi tu na si vinginevyo, hivyo vijana walipaswa kuunga mkono.
Imeandikwa na Leonce Zimbandu na Suleiman Msuya.
Hivyo makala Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni
yaani makala yote Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/polisi-yazuia-cuf-kufanyia-usafi-ofisi.html
0 Response to "Polisi yazuia CUF ‘kufanyia usafi’ ofisi Buguruni"
Post a Comment