Loading...

Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini

Loading...
Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini
link : Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini

soma pia


Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini

Na: Athumani Shariff

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa mkopo wa benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na kupeleka katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui, Shinyanga Vijijini na Nzega. 

Utekelezaji wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi, kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika mwezi Desemba 2015. 

Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya Shriram zote kutoka India. 

Sehemu ya tatu inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India. Usimamizi wa mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India. 

Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo na Visay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.
 Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
 Waziri wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora.



Hivyo makala Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini

yaani makala yote Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/prof-kitila-asaini-kandarasi-za-zaidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini"

Post a Comment

Loading...