Loading...

RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI

Loading...
RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI
link : RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI

soma pia


RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI

Rais John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ametangaza kuwafuta kazi watumishi 9,932 waliobainika kuwa na vyeti feki. Rais alisema "watu wote wenye vyeti feki waondolewe leo kwenye mfumo wa mishahara, wengine wanaojijua kuwa na vyeti feki wajiondoe wenyewe. Na ikifika tarehe 15 mwezi May wakiwa bado wanang'ang'ania huko ofisini muwakamate na wakafungwe hiyo miaka 7 kama waziri wa utumishi alivyosema na waonyeshe hao mawakala wa kutengeneza vyeti hivyo". Alisema hata wale 1176 wanaotumia cheti kimoja nao wazuiliwe mishahara ya mwezi huu mpaka itakapobainika nani ndio mwenye cheti chake.

Awali, akifafanua ripoti ya uhakiki wa vyeti, Waziri wa utumishi Mhe. Angela Kairuki alimshukuru Rais kukubali kutenga muda kwa ajili ya kupokea taarifa hii muhimu kwa mustakabali wa taifa letu. Mhe. Kairuki alisema mfumo wa mishahara maarufu kama Lawson kwa mwaka jana ulibaini vyeti 344 kati ya 1,114 vilivyowekwa kwenye mfumo huo kuwa zinatumiwa na watu zaidi ya mmoja au zaidi.

Mhe Angela Kairuki, waziri ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora


Mhe. Kairuki  alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa baraza la mitihani, ofisi za makatibu tawala mikoa na halmashauri na mashirika ya umma kwa kutumia muda mfupi kuhakiki jumla ya watumishi 435,000. 

Mhe. Kairuki alisema zoezi hili la uhakiki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa kama mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na madiwani kwasababu wao sifa zao za kuingilia ni kujua kusoma na kuandika kwa mujibu wa sheria.

Katika uhakiki huu, wamebainika watumishi katika makundi manne ambao ni wenye vyeti halali, vyeti feki, wanaotumia vyeti vyenye kufanana na wenye vyeti pungufu yaani wana vyeti vya taaluma lakini hawana vyeti vya kidato cha nne.

Mhe Kairuki alisema, kundi la kwanza ni la watumishi 376,966 sawa na asilimia 62.43 wamethibitishwa kuwa na vyeti halali. Kundi la pili ni watumishi 9,932 wamethibitika kuwa na vyeti feki. kundi la tatu ni lenye watumishi wanaotumia vyeti vinavyofanana na waliobadilisha maksi ya vyeti halali. Na kundi la nne na la mwisho ni watumishi 11,596 ambao wana vyeti pungufu yaani wana vyeti vya taaluma lakini hawana vyeti vya kidato cha nne hivyo uchunguzi bado unaendelea.

Akitoa salamu za utangulizi Waziri wa elimu sayansi na teknolojia, Mhe Joyce Ndalichako alimpongeza Rais kwa kusema " Mhe. Rais leo umeandika historia kwani tangu kuanzishwa kwa taifa hili wewe ndio umeagiza uhakiki ili watu wote wawe na sifa stahiki." 


Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia, Mhe Angela Kairuki


Ndalichako alisema " Mhe Rais tulipolipata agizo lako kupitia kwa waziri mwenye dhamana wa utumishi, tuliunda kikosi kazi cha watu 15, watu 10 wakitokea baraza la mitihani na watu 5 kutoka katika ofisi yako". Waziri Ndalichako aliwashauri wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wasipende njia za mkato na wasome kwa bidii kwani njia za mkato zimeshafungwa.



Hivyo makala RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI

yaani makala yote RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/rais-magufuli-awatumbua-watumishi-9932.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI AWATUMBUA WATUMISHI 9,932 WENYE VYETI FEKI"

Post a Comment

Loading...