Loading...
title : Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika
link : Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kugharamia Fursa za Elimu Duniani Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekamilisha ziara yake ya kuhamasisha utekekezaji wa Ripoti ya Kamisheni hiyo ijulikanayo kama 'Kizazi Cha Elimu' (The Learning Generation).
Katika ziara hiyo iliyomfikisha katika nchi 15, Rais Mstaafu Kikwete amekutana na Wakuu wa Nchi 12 wa nchi za Uganda, Malawi, Msumbiji, Congo, Tunisia, Ghana, Chad, Gabon, Ivory Coast, Namibia, Afrika Kusini na Botswana. Aidha amekutana na Makamu wa Rais wa Nigeria na Mawaziri Wakuu wa Ethiopia na Tanzania. Pamoja na viongozi wa nchi na Serikali, Rais Mstaafu amekutana na viongozi wa Taasisi za Kikanda 3 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Madhumuni ya ziara hizo yalikuwa ni kufikisha ujumbe wa Kamisheni na Ripoti yake juu ya umuhimu wa nchi za uchumi wa kati na chini (low and middle income countries) kufanya mapinduzi makubwa ya elimu ili kukabiliana na janga kubwa la elimu linaloinyemelea dunia.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Kamisheni hiyo, ubora wa elimu inayotolewa na nchi zinazoendelea za uchumi wa kati na chini ni ile ambayo imetolewa na nchi zilizoendelea miaka 70 iliyopita. Aidha, nchi zinazoendelea ziko nyuma sana katika vigezo vitatu muhimu vya elimu vya fursa ya kujiunga na elimu (access to education), kumaliza elimu (completion) na ufaulu na kuelimika (learning outcomes).
Hivyo makala Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika
yaani makala yote Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/rais-mstaafu-dkt-jakaya-kikwete_19.html
0 Response to "Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akamilisha Ziara ya Kamisheni ya Elimu kwa Kutembelea Nchi 15 Afrika"
Post a Comment