Loading...

TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA

Loading...
TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA
link : TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA

soma pia


TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA


 Image result for picha za manala


 Mwambawahabari
WAKATI Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikitarajia kukutana kesho jijini Dar es Salaam, uongozi wa vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba -
wameitahadharisha kamati hiyo kutokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa katika kufanya uamuzi kwenye ngazi mbalimbali.

Akizungumza  jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema klabu yake inasisitiza kila mwenye haki anatakiwa apatiwe kwa wakati unaofaa na kamwe si kuonyesha viashiria vya TFF kuzipendelea baadhi ya klabu au wanachama wa shirikisho hilo.


Manara alisema msingi wa kuheshimu vyombo vilivyopo unatakiwa kuheshimiwa huku pia akishangaa kuona Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inakutana kujadili uamuzi wa rufaa ya Simba wakati Kagera Sugar iliandika barua ya kuomba marejeo.

"Tunaomba haki itendeke, tunatoa tahadhari kuhusiana na kikao hicho, hatuoni uhalali wa kamati hiyo kukutana wakati Kagera Sugar katika barua yake imeomba uamuzi uliotolewa kufanyiwa marejeo, hii inatupa wasiwasi kuna nini hapa," alisema Manara.

Aliongeza kuwa sheria iko wazi inaeleza mtu, taasisi au klabu inapoomba hukumu ifanyiwe marejeo, basi kesi hiyo hupelekwa katika kamati au chombo kile kile na si vinginevyo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewataka viongozi wake kutokaa kimya endapo klabu hiyo itanyang'anywa pointi na kueleza kuwa msingi wa kuheshimu kanuni na sheria ndiyo unatakiwa kufuatwa na si matakwa au kusikiliza presha za upande wowote.

Kanuni ya bodi ya ligi namba 39 (5) (b na c) inaeleza kuwa mamlaka yenye uamuzi wa mwisho kufanya uamuzi ni Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Wakati huo huo ujumbe wa watu watatu wa Kagera Sugar jana ulianza safari kuja jijini kwa ajili ya kuitika wito uliotolewa na TFF wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji ambacho pia kitahudhuriwa na watendaji wa Bodi ya Ligi , waamuzi na kamisaa waliochezesha mchezo huo.

Katika kikao hicho, Kagera Sugar itawakilishwa na mratibu wa timu hiyo, Mohammed Hussein, kocha wa makipa na mchezaji Mohammed Fakhi ambaye anadaiwa kucheza akiwa na kadi tatu za njano katika mechi iliyoihusisha timu yake dhidi ya African Lyon.

Simba ndiyo ambayo inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 62, jana ndiyo ilipewa barua rasmi ya kuonyesha kushinda rufani yao dhidi ya Kagera Sugar iliyotolewa na Bodi ya Ligi.

Yanga inafuata katika msimamo huo ikiwa na pointi 56, lakini wana mechi mbili mkononi wakati Azam FC yenyewe ina pointi 46 na Kagera Sugar ni ya nne ikiwa na pointi 43


Hivyo makala TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA

yaani makala yote TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/tff-yapewa-onyo-na-simba-kuhusu-point.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TFF YAPEWA ONYO NA SIMBA KUHUSU POINT ZA KAGERA"

Post a Comment

Loading...