Loading...
title : WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.
link : WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.
WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.
Na Ripota wetu Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbali mbali ya kihalifu pamoja na dawa za kulevya, Unyang'anyi wa kutumia Silaha katika Maeneo Mbali Mbali ya Jiji La Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Saimon Sirro amesema Operesheni hiyo ni endelevu na Jumla ya kete 366 za dawa zakulevya zimekamatwa pamoja na puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.
Aidha Sirro amesema kuwa Operesheni Kali ya kuwasaka wahalifu wa Makosa hayo mbali mbali ikiwemo kosa la kupatikana na Dawa za kulevya bado inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu.
" Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea Kuhojiwa Kulingana na Makosa yao na pindi Upelelezi Utakapokamilika Watafikishwa Mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.
Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa Mnamo tarehe 15 Mwezi huu 2017 Majira ya Saa moja Usiku Maeneo ya kiwalani kwa Ally Mboa, Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Silaha Moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na Mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.
" Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika Maeneo hayo ambapo Walisikia harufu ya bhangi na kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea na ndipo Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Saimon Sirro akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na watuhumiwa waliokamatwa kwa Makosa mbali mbali ya kiharifu.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Saimon Sirro akionesha baadhi ya vitu mbali mbali walivyo vikamata.
Hivyo makala WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.
yaani makala yote WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/watuhumiwa-267-wakamatwa-jijini-dar-es.html
0 Response to "WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI."
Post a Comment