Loading...

WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA

Loading...
WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA
link : WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA

soma pia


WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA


Na Veronica Simba – Dodoma

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa wito kwa wataalam nchini, hususan walioko katika sekta za mafuta na gesi kulisaidia Taifa kuepukana na mikataba mibovu kwa kutumia utaalam wao badala ya wao kuendelea kulalamika kama wananchi wa kawaida.

Profesa Muhongo alitoa wito huo jana, Aprili 27, 2017 wakati akizindua Bodi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi hiyo, Profesa Muhongo alisema kwamba, kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wananchi kuhusu Taifa kuibiwa rasilimali mbalimbali na makampuni ya kigeni kutokana na mikataba mibovu iliyoingiwa awali.

“Ni kwa sababu hiyo, uteuzi wa wajumbe wa Bodi hii ya PURA, umezingatia sifa za hali ya juu za kitaaluma mlizonazo, ili pamoja na mambo mengine muweze kulisaidia Taifa kunufaika ipasavyo na rasilimali hizi adhimu za mafuta na gesi, kwa kuhakikisha mikataba inayoingiwa, inakuwa yenye manufaa kwetu.”

Akifafanua zaidi, alisema kuwa, Bodi ya PURA ina wajumbe watano ambao wamebobea katika taaluma za sheria, fedha, uhasibu na mazingira; sifa ambazo zinaifanya Bodi hiyo kuwa miongoni mwa Bodi bora kabisa hapa nchini.

Aliwataka wataalam hao kuachana na kasumba ya kulalamika kuwa Taifa linaibiwa badala yake watumie utaalam na ubobezi wao kuhakikisha changamoto hiyo inabaki kuwa historia nchini hususan katika sekta wanayoisimamia.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) iliyofanyika Aprili 27, 2017 makao makuu ya Wizara mjini Dodoma.
 Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Habass Ng’ulilapi (kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe), akiwasomea majukumu yao, wajumbe wa Bodi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA), katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, iliyofanyika makao makuu ya Wizara mjini Dodoma.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) iliyofanyika Aprili 27, 2017 makao makuu ya Wizara mjini Dodoma.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiwakabidhi vitendea kazi baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA), mara baada ya kuizindua rasmi katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Wizara mjini Dodoma.



Hivyo makala WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA

yaani makala yote WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/waziri-muhongo-awataka-wataalam.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATAALAM KULISAIDIA TAIFA"

Post a Comment

Loading...