Loading...

ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU

Loading...
ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU
link : ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU

soma pia


ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU

Na: Martin Mhina

Leo nigusie baadhi ya vitu vya kuzingatia kwa ajili ya ufugaji bora wa kuku.

UFANISI WA UFUGAJI WA KUKU BORA HUTEGEMEANA NA MAMBO YAFUATAYO;

  1. Ujenzi wa banda bora kwa kuzingatia vipimo sahihi
  2. Uchaguzi wa kuku wazazi wenye sifa nzuri
  3. Udhibiti na tiba za magonjwa mbalimbali kwa kuzingatia Ratiba sahihi za chanjo
  4. Ulishaji bora kwa waakati na Chakula kiwe na viin lishe vyote
  5. Uzingatiaji Wa usafi Wa banda na vyombo

A.  SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

  • Liingize mwanga na hewa muda wote
  • Liwe Kavu daima
  • Liwe na nafasi ya kutosha kuanzia vipimo vya upana 3M na urefu 4/5M kuku wasibanane
  • Liwe la Gharama Nafuu lakin la kudumu unaweza ukatumia Mabanzi, mbao, mianzi, matofali katika ukuta na paa tumia Vigae, Bati na nyasi
  • Liielekeze kuzuia upepo na mvua pia kuzuia wanyam na wadudu hatari kwa Kuku
  • Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya Chakula na ndani kuwe na maranda, bembea, vichanja
  • Kuwe na Uzio mpana angalau mita 10*12 ili wapate mahala paa kuota joto

 B. ILI KUEPUKA VIFO VYA KUKU FANYA YAFUATAYO
  • Osha banda na vyombo kwa dawa kama V-RID kila baada ya miezi 3/6 ili kuua bacteria nk
  • Chanja kuku chanjo zifuatzo Mahepe (Mareks ) kuanzia siku Ya 1-3 ,Mdondo siku 3-7 utarudia siku Ya 21,Gumboro siku 14 na Ndui siku ya 28 NOTE chanjo zote hizi utarudia kila baada ya miezi 3
  • Wape Vitamin Kama Multivitamin, vitalstress au maji ya molasses Ya unga
  • Usafi Wa banda ni muhimu Epuka watu kuingia bandani ukiweza kuwe na mavazi maalumu kama Ovaloli, maganbut zitazo fuliwa kwa dawa maalumu kwa ajili ya mfanyakaz na wagen wanaotembelea
C. EPUKA MAADUI HAWA HATARI KWA MIFUGO KAMA NYOKA, KENGE, PAKA, PANYA, MMBWA, KICHECHE NK KWA KUTUMIA MBINU ZIFUATAZO
  • Mwaga mafuta ya Dizel pamoja na mchanga zunguushia pembeni ya banda nyoka na kenge hatosogea
  • Chemsha mayai kisha yatege mahali Kuanzia mbwa, paka, nyoka, kenge, kicheche, akimeza lazima afe maana yai halitavunjika
  • Chimba shimo refu kidogo pemben ya kibanda au katikati kisha weka pumba, panya, mende, paka wamedumbukia ukiongeza na dagaa kidogo
D. ZUNGUSHIA UA WA MTI WA NNYOKA (Mnyonga pembe )KAMA UZIO WA BANDA AU SHAMBA LA MIFUGO PEMBENI KWENYE MIPIKA

Mti huu harufu yake hufukuza na kudhibiti KENGE NA NYOKA hata mwizi akitaka kuiba huwa mashaka ya kukamatwa pia mtii huu Majani yake /Magome yake yakipondwa.

Husaidia kuponya mtu aliyengatwa/kutemewa mate na nyoka Pia husaidia kuku aliye dumaa au mwenye minyoo kumboost Mti huu hupandwa Kama muhogo Na unapatikana Tanga kila bando la miche 18 unalipia elfu 20.


Ukihitaji miti hii au kwa msaada piga no 0625564876

Picha mbalimbali za kuku na mabanda








 







 



Hivyo makala ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU

yaani makala yote ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/zijue-baadhi-ya-mbinu-za-ufugaji-bora.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ZIJUE BAADHI YA MBINU ZA UFUGAJI BORA WA KUKU"

Post a Comment

Loading...