Loading...
title : Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,
link : Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,
Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,
Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba, Zanzibar, Tanzania
Assalaamu Alaykum warahmatuLlaahi wabarakaatuh
Mwezi mtukufu wa Ramadhaan umekaribia. Kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha nchini Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla umeleta uharibifu mkubwa wa nyumba, miundo mbinu, mashamba na vipando.
Kuna ndugu zetu watakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan kutokana na maafa haya.
Jumuiya ya Al Iman ya Northamptonshire nchini Uingereza imeamua kuwasaidia waathirika wa maafa haya hasa kisiwani Pemba kwa kuanzisha “Kikapu cha Ramadhaan” (Ramadhaan Basket) ambapo ndani yake mtakuwa na vitu muhimu kama mchele, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kupikia na majani ya chai na kadhalika
Kwa Pauni £25.00 tu unaweza kujipatia kikapu chako na mchango wako angalau kuwapunguzia ukali wa maisha ndugu zetu walioathirika na maafa hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
Tunakuomba kwa moyo mkunjufu, andaa kikapu chako sasa na atakulipa kwa mchango wako kwa kuchangia Pauni 25.00 tu kwa kikapu kimoja. (unaweza kuongeza vikapu zaidi ukihitajia)
Al Iman Society of Northamptonshire ni Jumuiya iliyosajiliwa kama Jumuiya ya khiari yenye makaazi yake Northampton ikiwa na namba ya usajili 1117020
Kutuma mchango wako, Lloyds Bank sort code 309609 Account 03539228
Tumia reference: ‘Ramadhaan Basket’
Kama utachangia kwa njia ya cheki hakikisha cheki imeandikwa na kulipwa kwa Al – Iman Society of Northamptonshire. Na upande wa nyuma iandikwe: ‘Ramadhaan basket’
Au unaweza kutuletea kwenye Msikiti wetu: Northampton Mosque & Islamic Centre, Clare Street, Northampton NN1 3JF England
Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi wasiliana na Amiyr wa Jumuiya: Ustaadh Abdulrazak +44 7951816208 au email iman@al-iman.co.uk
Baaraka Llaahu fiykum
Hivyo makala Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,
yaani makala yote Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba, mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/agizia-kikapu-chako-cha-ramadhaan.html
0 Response to "Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,"
Post a Comment