Loading...

AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING

Loading...
AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING
link : AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING

soma pia


AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za kupata ajali kwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting FC iliyotokea leo barabara ya Manyoni mkoani Singida wakati kikosi hicho kikitokea Shinyanga kwenda Pwani.

Taarifa kutoka Singida zinasema gari hilo lilipata ajali baada ya kupasuka tairi moja la mbele hivyo kuyumba na kuacha njia eneo la Itigi - kilometa 200 kutoka Singida mjini kuelekea Manyoni hivyo kutoka barabarani kuu kabla ya kugonga mti.

Taarifa hizo zilizothibitishwa na Masau Bwire, zinasema wachezaji watatu akiwamo Bwire mwenyewe ndio waliopata majeraha na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Singida kwenda kutibiwa. Wachezaji hao ni Yussuf Nguya, Abdul Mpambika na Saidi Dilunga.

Timu hiyo ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao 2-1, hata hivyo imebaki kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao baada ya kushika nafasi ya saba. 

Mara baada ya kupata taarifa hizo, Rais wa TFF Jamal Malinzi mara moja ametuma salamu za kuwapa pole uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania pamoja na timu nzima ya Ruvu Shooting.

“Nawapa pole viongozi wote, makocha na wachezaji. Na kwa wachezaji ambao wamejeruhiwa na viongozi wote waliojeruhiwa akiwamo ndugu yetu Masau Bwire, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka,” amesema Malinzi.

Rais Malinzi alimshukuru Mungu kwa kuepusha vifo kwa wanafamilia hao wa mpira wa miguu hasa wakati huu Watanzania wakiwa makini kufuatilia maendeleo ya timu za taifa.


Hivyo makala AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING

yaani makala yote AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/ajali-rais-malinzi-awafariji-ruvu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AJALI: RAIS MALINZI AWAFARIJI RUVU SHOOTING"

Post a Comment

Loading...