Loading...

Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha

Loading...
Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha
link : Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha

soma pia


Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha


Leonce Zimbandu

MKAZI wa Kipunguni, Ilala, Obadia Mtawa, amemtelekeza mkewe, watoto wanne na kwenda kusikojulikana kutokana na ugumu wa maisha.

Tukio hilo lilifahamika baada ya Nuru Khasim kuzungumza na mwandishi wa gazeti hili jana kuhusu mumewe huyo kumtelekeza na kutoweka na yeye kutangatanga na watoto.

Alisema ni mwaka mmoja sasa tangu Mtawa aikimbie familia yake, hivyo anaendelea kuteseka huku akikosa msaada wa ndugu kutokana na tabia mbaya ya ndugu yao.

“Nimevumilia kwa muda mrefu kwani siku moja wakiwa na rafiki yake walininyonga mkono na kuvunja kijiti nilichoweka mwilini kuzuia kushika mimba,” alisema.

Alisema baada ya ukatili huo alilazimishwa kufanya mapenzi na kushika ujauzito na kujifungua kwa njia ya operesheni na kukosa msaada kwa vile mumewe alitoweka.

Aliongeza, kuwa kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu, alikwenda ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Kipunguni kulalamika ili kupata msaada wa malezi.

Ofisa Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Kipunguni, Clement Sinda alisema  ofisi hiyo ilipokea malalamiko ya Nuru, na inaendelea kutafiti kwa kushirikiana naye ili kumpata mumewe.

“Tunahitaji kupata taarifa za eneo analoishi sasa ili iwe rahisi kufanya mawasiliano na ofisa ustawi wa jamii wa eneo hilo, ili akamatwe na kurudishwa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema  ofisi hiyo inaendelea pia kumtafuta rafiki  wa Mtawa aliyeshiriki kumpiga na kumnyonga mkono Nuru na kuvunja kijiti alichoweka cha uzazi wa mpango.

Mwandishi wa habari hizi alipompigia simu Mtawa huku akisita kutaja anakoishi, alisema alitoweka Dar es Salaam kutokana na ugumu wa maisha na yuko Morogoro akijishughulisha na kilimo.

“Sijamtelekeza, bali ni ugumu wa maisha, tayari nimelima mpunga na mahindi, nitarudi kuchukua familia yangu,” alisema.


Hivyo makala Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha

yaani makala yote Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/atelekeza-familia-kwa-ugumu-wa-maisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Atelekeza familia kwa ugumu wa maisha"

Post a Comment

Loading...