Loading...

BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE

Loading...
BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE
link : BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE

soma pia


BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE

Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.


Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.

Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yao waliyoianzisha. 

Bwana Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua miradi ya Tasaf.
Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.  Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).  Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji.



Hivyo makala BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE

yaani makala yote BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/balozi-seif-akutana-na-ujumbe-wa-benki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE"

Post a Comment

Loading...