Loading...
title : Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo
link : Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo
Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo
BENKI ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia.
Alisema kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara, James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha katika kuendeleza biashara zao.
Alisema Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'.
Hivyo makala Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo
yaani makala yote Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/benki-ya-nmb-yazinduwa-fanikiwa-account_25.html
0 Response to "Benki ya NMB yazinduwa 'Fanikiwa Account' kwa wafanyabiashara wadogo"
Post a Comment