Loading...
title : Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge
link : Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge
Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge
Mwandishi Wetu
Jaji Semistocles Kaijage |
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi ya ubunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema kuwa wazi.
Uamuzi huo umekuja baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Dk Elly Macha, aliyefariki dunia Machi 31.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, alitangaza nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343.
“Tayari Spika wa Bunge ameijulisha Tume juu ya kuwepo kwa nafasi wazi ya mbunge huyo,” alisema Jaji Kaijage.
Alisema taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Dk Macha alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu bungeni hadi alipofariki dunia akiwa Uingereza kwa matibabu.
Hivyo makala Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge
yaani makala yote Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/chadema-yawa-rasmi-na-pengo-la-mbunge.html
0 Response to "Chadema yawa rasmi na pengo la mbunge"
Post a Comment