Loading...

DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI

Loading...
DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI
link : DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI

soma pia


DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI

Mwambawahabari
MAGAR1
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Manyara Eng. Bashiri Rwesingisa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua mahali ambapo litajengwa Daraja la Magara lenye urefu wa Mita 84, Wilayani Babati, mkoani Manyara, jana.
MAGAR2
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Christopher Saul (katikati), kutoka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), mkoa wa Manyara wakati alipokuwa akikagua mahali ambapo litajengwa Daraja la Magara lenye urefu wa Mita 84, Wilayani Babati, mkoani humo, jana.
MAGAR3
Muonekano wa Sehemu ambapo Daraja la Magara lenye urefu wa Mita 84 katika barabara ya Mbuyu wa Mjerumani-Mbulu KM 21 litakapojengwa. Mkataba wa ujenzi wake unatarajiwa kusainiwa mwezi Juni mwaka huu.
MAGAR4
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mayoka kuhusu mkakati wa Serikali katika ujenzi wa Daraja la Magara wilayani Babati, mkoani Manyara, jana.

…………………………………………………………………..
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga Daraja la Magara lenye urefu wa Mita 84 katika barabara ya Mbuyu wa Mjerumani-Mbulu KM 21 lililopo mkoani Manyara ambapo mkataba huo unatarajiwa kusainiwa mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza hayo jana kwa wananchi wa Kijiji cha Mayoka, wilaya ya Babati, mkoani humo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa mkandarasi atakayepatikana ili kurahisisha mradi huo kukamilika kwa wakati.
“Serikali inaendelea kukamilisha taratibu zake ili kumpata mkandarasi, sasa ombi langu kwenu ni kuhakikisha kuwa mnatoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo pindi atakapofika eneo la kazi”, amesema Naibu Waziri.
Amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikitenga fedha mwaka hadi mwaka ili kuweza kukamilisha mradi huo ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/18 zaidi ya Shilingi Bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa KM 1.2 za barabara sehemu ya mlima Magara ambayo itajengwa kwa kiwango cha zege.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Manyara Eng. Bashiri Rwesingisa amemhakikishia Naibu Waziri huyo kumsimamia mkandarasi atakayepatikana katika ujenzi wa Daraja hilo ili kuondoa kero na adha wanayopata wakazi wa Babati na maeneo jirani.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Daraja la Magara pia litahusisha ujenzi wa barabara unganishi zenye urefu wa KM 2 kwa kiwango cha lami na KM 2 kwa kiwango cha Changarawe.
Daraja la Magara ni moja ya Daraja litakaloleta chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Arusha, Mbulu na Babati kwani ujenzi wake utarahisisha huduma za usafirishaji na kukuza utalii kwa nchi kupitia Hifadhi ya Mbuga ya Manyara.


Hivyo makala DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI

yaani makala yote DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/daraja-la-magara-kuanza-kujengwa-mwezi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI"

Post a Comment

Loading...