Loading...

Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

Loading...
Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha
link : Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

soma pia


Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

Mwambawahabari
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8-May-2017 ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.


Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.

Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga miili ya ndugu zao leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent.

Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent waliofariki kwenye ajali.


Hivyo makala Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

yaani makala yote Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/makamu-wa-rais-aongoza-watanzania-kuaga_31.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha"

Post a Comment

Loading...