Loading...
title : MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA
link : MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA
MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA
MwambawahabariNa Richard Mwaikenda, Mtama
WALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.
Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.
Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.
Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.
Pia aliwashauri akina baba na kaka kutokuwa mbali na wasichana kwani nao ni wajibu wao kuwasaidia na ikiwezekana kuwapatia msaada wa hali na mali ikiwemo kuwanunulia vifaa vinavyowafaa wakiwa hedhi.
Mwalimu Mariamu Hashima wa Shule ya Msingi Lihimba, aliiisifia kampeni hiyo kwa kuendeshwa kwa uwazi na ukweli, lakini alishauri kuwa mafunzo hayo yatenganishwe kwa watoto wa shule za msingi kuwafundisha zaidi jinsi ya kujiandaa kupata hedhi na vifaa anavyopaswa kuwa navyo.
Timu ya kampeni hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, Mkufunzi Msaidizi Rehema Kijazi, Kiongozi wa Girl Guides Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango.
Hivyo makala MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA
yaani makala yote MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/mtama-waifagilia-kampeni-ya-tgga-ya.html
0 Response to "MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA"
Post a Comment