Loading...
title : Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala
link : Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala
Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala
Joyce Kasiki, Dodoma
Ummy Mwalimu |
SERIKALI imesema asilimia 60 ya Watanzania wanategemea tiba inayotolewa na waganga wa tiba asilia.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (CCM) aliyeihoji Serikali kwa nini haitambui mchango wa waganga hao na ikawapa elimu ya masuala ya afya.
"Hivi siku zote watu wamekuwa wakiwasemea wasanii kwamba wanatumika wakati wa uchaguzi na baada ya hapo wanasahaulika,lakini kwa kipawa nilichonacho na nikiangalia humu ndani (Bungeni) ,wabunge wote mnaonekana mmepita kwa waganga hawa kama hawapo labda wawili au watatu,kwani Serikali haitoi elimu kwa kundi hili ambalo limekuwa kimbilio la watanzania?" alihoji Kasheku
Akijibu swali hilo, Ummy alisema Serikali inatambua mchango wa watu hao kwa kuwa kundi kubwa linawategemea waganga hao wa tiba mbadala.
Mapema katika swal la msingi Mbunge wa Ushetu Elias Kwandikwa (CCM) alitaka kujua ni waganga wangapi wa kienyeji wamekamatwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kufuatia msako ambao umekuwa ukifanywa na jeshi hilo.
Akijibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuf Masauni alisema,waganga wa kienyeji waliokamatwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ni 26 na kushitakiwa kutokana na kufanya biashara ya uganga bila kibali na kupatikana na nyara za Serikali.
"Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya waganga 16 walikamatwa na kufikishwa mahakamani ,Kati ya hao waganga saba walipatokana na hatia kwa kufungwa miaka miwili kila mmoja au kulipa faini ." alisema Masauni
Alisema,jumla ya watuhumiwa sita katika kesi tofauti walilima faini ya jumla sh.milioni 1.25, mtuhumiwa wa kesi moja alihukumiwa miaka miwili bila yeye kuwepo mahakamani ambapo juhudi za kumsaka zinaendelea.
Hivyo makala Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala
yaani makala yote Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/nusu-ya-watanzania-wanatumia-tiba.html
0 Response to "Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala"
Post a Comment