Loading...
title : RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU
link : RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU
RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU
Rais Mahmuud Abbas wa Palestina amesema kwamba,Matakwa ya wafungwa wa kipalestina walio katika jela za Israeli ni ya haki na ni wajibu wa Israli kuyatekeleza, vilevile kupatikana kwa uhuru wa taifa lake ndio ufunguo wa amani na utulivu katika ukanda huo wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima kwa ujumla.
Rais Abbas ameyasema hayo jana Jumanne Ikulu mjini Beit Lehem, alipokuwa na mkutano wa pamoja na mgeni wake Rais Donald Trump wa Marekani, huku akitilia mkazo dhamira yake ya kushirikiana nae katika kufanikisha mpango wa amani wa kihistoria na Waisraeli,pia kushirikiana nae Rais Trump kama washirika katika suala zima la kupiga vita Ugaidi duniani.
Mheshimiwa Rais Mahmuud Abbas pia ametilia mkazo msimamo wa Palestina unaotegemea utatuzi wa uwepo wa dola mbili chini ya mipaka ya mwaka 1967, ambazo ni dola ya Palestina ikiwa na mji mkuu wake Jerusalemu ya Mashariki na dola ya pili ni Israeli,huku ukipatikana utatuzi wa mwisho kabisa wa masuala yote husika, kwa misingi ya maazimio ya kisheria za kimataifa na makubaliano ya pande mbili za Palestina na Israeli.
Aidha Rais Abbas ametilia mkazo pia kwamba mzozo uliopo sio wa kidini,kwani kuheshimu dini zote na mitume yake ni sehemu ya imani ya taifa la Palestina, bali tatizo lililopo ni uvamizi, ujenzi wa makazi ya walowezi na kutokubali Israeli uwepo wa dola ya Palestina.
Rais Abbas pia amezungumzia usumbufu wanaoupata wafungwa wa kipalestina wanaoendelea na mgomo wa kula uliofikisha siku 37 mfululizo katika jela za Israeli,huku akitilia mkazo ya kwamba madai yao ni ya kibinaadamu na ya haki,ni wajibu wa Israeli kuyatekeleza.
Kwa upande mwingine,Rais Abbas amelaani vikali shambulio baya la kigaidi, lililotokea hivi karibuni mjini Manchester Uingereza lililopelekea vifo kadhaa na majeruhi,huku akitoa rambirambi zake za dhati kabisa kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na familia za wahanga hao.
Rais mahmuud Abbas na mwenzake Donald Trump,wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Beit Lehem.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU
yaani makala yote RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/rais-abbas-uhuru-wa-palestina-ndio.html
0 Response to "RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU"
Post a Comment