Loading...
title : Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja
link : Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja
Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi utakaosaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Lazaro Kitandu alisema uamuzi huo wa kuanzisha mfumo mpya umekuja baada ya Serikali kugundua kuwa kwa muda mrefu matumizi ya mbolea hapa nchini si ya kuridhisha kutokana na bei ya mbolea kuwa juu.
“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mbolea imeanzisha mfumo huu baada kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam waelekezi wa ndani na nje ya nchi na kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja” Alisema Kitandu.
Kitandu alieleza kuwa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA), Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye matumizi ya chini ya mbolea kwa kutumia kilo 19 za virutubisho hivyo kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo ambapo kiasi hicho hakiendani na malengo ya azimio la Maputo la nchi za SADC linalotaka kufikia angalau kilo 50 kwa hekta moja.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga. Picha na Fatma Salum- MAELEZO
Hivyo makala Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja
yaani makala yote Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/serikali-yaanzisha-mfumo-wa-ununuzi-wa.html
0 Response to "Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja"
Post a Comment