Loading...
Loading...
- Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa , tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title :
link :

soma pia


Taasisi na Asasi Zisizokuwa za Kiserikali za Tanzania (NGOs) taasisi za serikali zinazoshughulikia uwajibikaji na wadau wengine kadhaa walikutana hivi leo  ili kufanya tathmini ya hatua zilizopigwa na mafunzo yaliyopatikana wakati wa uhai wa mradi wa Pamoja Twajenga  unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Toka mwaka 2013, watendaji wa mradi wa Pamoja Twajenga wamekuwa wakifanya kazi bega kwa bega na asasi za kiraia na taasisi za serikali ya Tanzania zinazoshughulikia masuala ya uwajibikaji ili kuimarisha mahusiano kati ya asasi za kiraia na serikali. Mradi huu ulitoa mafunzo na msaada kwa jumla ya asasi zisizo za Kiserikali 16 na taasisi tatu za serikali zinazojihusisha na uwajibikaji katika mikoa ya Mtwara, Iringa, Dodoma, Morogoro na  Zanzibar kwa lengo la kukuza uwazi na uwajibikaji wa serikali kwa raia wa Tanzania. 
Kutokana na msaada huu, hivi sasa asasi za kiraia na taasisi za uwajibikaji zilizoshiriki zina uwezo zaidi wa kushiriki katika mijadala kuhusu masuala mahsusi yanayozigusa jamii (issue-based dialogue).
Raia katika mikoa lengwa ya mradi – ikiwa ni ni pamoja na vijana, wanawake na makundi mengine ya watu wanaowekwa pembezoni wana uwezo zaidi wa kujadiliana na serikali zao kuhusu kero zao, jambo ambalo limeongeza uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa rasilimali za umma na katika ufanyaji maamuzi
. Asasi za kiraia zilizosaidiwa na mradi wa Pamoja Twajenga zinafanya kazi katika masuala yanayohusiana moja kwa moja na mahitaji ya msingi ya raia ikiwa ni pamoja na huduma za afya, elimu, usalama wa chakula na usimamizi wa rasilimali. 
 Majadiliano ya jumuiya katika kata ya Mpapula mkoani Mtwara, mwanajamii akielezea uzoefu wao kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto. Majadiliano hayo yaliandaliwa na asasi ya kiraia ya Wanasheria Wanawake Katika Maendeleo Afrika (Women in Law and Development in Africa - WiLDAF), mojawapo kati ya asasi za kiraia zilizopokea msaada kutoka mradi wa Pamoja Twajenga uliokuwa ukifadhiliwa na USAID. (Picha kwa hisani ya: Rhoda Nashon/WiLDAF)
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA



Hivyo makala

yaani makala yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/taasisi-na-asasi-zisizokuwa-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to " "

Post a Comment

Loading...