Loading...
title : Taasisi yajadili bajeti ya nchi
link : Taasisi yajadili bajeti ya nchi
Taasisi yajadili bajeti ya nchi
Mwandishi Wetu
Dk Tausi Kida |
TAASISI ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imekutanisha wadau wa maendeleo nchini kujadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/17 ambao unaelekea ukingoni.
Akizungumza katika mkutano huo juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida, alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli zinazofanywa na ESRF ili kutazama ni jinsi gani taasisi hiyo inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Dk Kida alisema mdahalo huo unahusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/18.
“ESRF imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo tofauti,” alisema Dk Kida.
Aliongeza: “Kama jinsi mnavyojua nchi yetu imekuwa na mipango ya maendeleo inayotekelezwa kupitia bajeti kwa kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo kwa nchi.”
Mwakilishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Joviter Katabaro ambaye ni Mkufunzi wa Shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema pamoja na Serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani, lakini bado kuna changamoto katika elimu zinazohitaji kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya mwaka 2017/18.
“Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule, upungufu wa maktaba 15,000 na vyoo bado havitoshi,” alisema Dk Katabaro.
Profesa Haidari Amani, Mtafiti Mshiriki Mwandamizi (ESRF) aliyetoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto, Serikali inatakiwa kuweka mfumo mzuri kuanzia wakulima wadogo ili kunufaika na kilimo.
Hivyo makala Taasisi yajadili bajeti ya nchi
yaani makala yote Taasisi yajadili bajeti ya nchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi yajadili bajeti ya nchi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/taasisi-yajadili-bajeti-ya-nchi.html
0 Response to "Taasisi yajadili bajeti ya nchi"
Post a Comment