Loading...

TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR

Loading...
TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR
link : TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR

soma pia


TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR




Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imeanza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo visiwani Zanzibar kwa kuanza mchakato wa kutoa mikopo kwa wakulima na wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha katika uchakataji wa mazao ya kilimo visiwani humo. 

Akizungumza wakati wa walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, visiwani humo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

“Uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi  Maryam Juma Abdullah (aliyesimama) akiwakaribisha ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB). 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi  Maryam Juma Abdullah (aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ulipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Ugeni huo upo visiwani Zanzibar kuangalia maeneo ya uwekezaji visiwani humo. 

Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (wapili kushoto) na Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia). 
Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR

yaani makala yote TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/tadb-yabisha-hodi-visiwani-zanzibar.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR"

Post a Comment

Loading...