Loading...
title : TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama
link : TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama
TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama
MwambawahabariWafanyakazi wa kiwanda cha Darbrew cha jijini Dar es Salaam, (kinachozalisha kinywaji cha Chibuku ) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kiwanda hicho Tito Kasele wakati wa semina ya masuala ya usalama mahali pa kazi.
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Zima Mota na Uokoji Peter Mwambene akitoa elimu juu ya kujikinga na majanga ya moto kwa wafanyakazi wa TBL Ilala jijini Dar es salaam
Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifuatilia mafunzo ya usalama
Wafanyakazi wa kampuni ya Konyagi wakifuatilia mafunzo ya usalama
Waziri wa Sera,Bunge,Vijana,Ajira na Walemavu,Jenista Mhagama,akipata maelezo ya kanuni za usalama za kampuni wa TBL Group kutoka kwa Meneja Usalama wa TBL Group (TBL Safety Manager),Renatus Nyanda,wakati walipotembelea banda ya maonyesho ya Wiki ya Usalama mahali pa kazi yaliyomalizika katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
Meneja Usalama wa TBL Group,Renatus Nyanda akitoa maelezo ya usalama kwa wananchi waliotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakisikiliza mada ya usalama kutoka kwa afande Muganyizi kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani.
……………
Kampuni ya TBL Group imeweka mikakati kuhakikisha viwanda vyake vyote nchini vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama mahali pa kazi na nje ya kazi kwa viwango vya kimataifa.
Akiongea wakati wa kilele cha wiki ya Usalama mahali pa kazi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni iliandaa mafunzo mbalimbali ya Usalama kwa wafanyakazi wake na kushiriki maounyesho ya usalama mahali pa kazi yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro,Meneja wa Usalama na Afya kwa TBL,Renatus Nyanda,alisema kuwa usalama sehemu za kazi ni moja ya suala ambalo kampuni inalipa kipaumbele kikuu na kuhakikisha hakujitokezi matukio ya ajali maeneo ya kazi.
“Usalama ni suala tunalolipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa bila kuwepo usalama sehemu za kazi ni vigumu kufanya kazi kwa ufanisi na ndio maana tunashikilia rekodi ya kushinda tuzo ya Usalama Mahali pa Kazi inayotolewa na taasisi ya Tanzania Occupational Health and Safety Agency (OSHA) na tuzo ya shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA)”
Alisema kampuni kutokana na suala la usalama kupewa kipaumbele matukio ya ajali yamekuwa yakipungua mwaka hadi mwaka katika shughuli za uzalishaji viwandani kwa kuwa kila mfanyakazi amefundisha kulinda usalama wa kwake binafsi na wenzake na usalama huo umekuwa hauishii kwa wafanyakazi tu bali na wakandarasi na wageni wanaotembelea maeneo ya kampuni usalama wao unazingatiwa.
Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa jinsi wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na kampuni ikiwemo kufunga mashine za kisasa hali ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda vilivyopo chini ya TBL Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na viwanda vingine nchini
Katika maadhimisho ya Wiki ya Usalama Kazini iliyofikia kilele mwishoni mwa wiki wafanyakazi wote wa kampuni ya TBL Group walihudhuria semina mbalimbali za ndani zilizoendeshwa na wataalamu kutoka taasisis mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kuhusiana na masuala ya usalama mahali pa kazi.Viwanda vya kampuni ya TBL Group hapa nchini vipo katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
Hivyo makala TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama
yaani makala yote TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/tbl-group-yaadhimisha-wiki-ya-usalama.html
0 Response to "TBL Group Yaadhimisha Wiki Ya Usalama Sehemu Ya Kazi Kwa Vitendo-Wafanyakazi Wapatiwa Mafunzo Ya Usalama"
Post a Comment