Loading...

WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI

Loading...
WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI
link : WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI

soma pia


WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI

Magere Mugeta mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amegawa hati miliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara yake mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.

Wananchi hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi. Hata hivyo jumla ya wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa ajili ya urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha michango stahili.

Katika ziara hiyo, waziri Lukuvi amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo na kugundua kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi 28,000 wameishapelekewa hati ya madai.

Waziri Lukuvi pia ametembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya kumbukumbu za wananchi kuhusu taarifa za ardhi ikiwemo masuala ya hati na kukugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi. Mmoja ya viongozi hao ni Mbunge wa Kwimba Shannif Mansoor ambaye hajalipa kodi ya pango la ardhi tangu 2010 kiasi cha shilingi milioni 529.

Aidha katika wilaya hiyo ameongea na wananchi wa Nundu kata ya Meko, mbali ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo, amewahimiza kuchamkia fursa ya kurasimisha makazi yao na kupata hati ili kuzipa thamani ardhi zao na kujitanulia fursa za uchumi.
Janet Magige mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiwasisitiza wakazi Lamadi mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki ardhi kwa hati kwa kuwaonesha moja ya hati zinazotolewa kwa wananchi.
Wakazi wa Lamadi mkoani Simiyu wakishangilia pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuwawezesha kupata Hati za kumiliki Ardhi.



Hivyo makala WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI

yaani makala yote WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wakazi-122-mkoani-simiyu-wapewa-hati-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI"

Post a Comment

Loading...