Loading...

WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO

Loading...
WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO
link : WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO

soma pia


WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO


Na; Elinipa Lupembe

Wamiliki wa shule binafsi wilayani Arumeru  wamepewa siku hamsini mpaka kufikia tarehe 15.07.2017 kuhakikisha wanalipa madeni yao ya kodi wanazodaiwa na Shirika la Mapato Tanzania 'TRA'.      
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Alexander Mnyeti alipokutana na wamiliki wa shule binafsi  73 za msingi na sekondari zinazoendeshwa  katika wilaya ya Arumeru alipokutana nao   kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Meru.                        
Mkuu wa wilaya Mnyeti amesema amelazimika kuwaita baada ya kufuatilia na kuona shule nyingi binafsi hazilipi kodi ya serikali kwa kivuli cha kuwa wanatoa huduma.
"Nyinyi wamiliki wa shule hamlipi kodi ya serikali kwa kivuli cha kutoa huduma lakini nimefanya utafiti na kugundua  mnatoza ada  kubwa kati ya milioni moja na nusu mpaka milioni  tatu  kifupi hiyo ni biashara sio huduma "alisisitiza Mnyeti.
                   
Mnyeti amewaelekeza wamiliki wa shule hizo binafsi kuwa shule inayotoa  huduma mwanafunzi anatakiwa kulipa ada elekezi ya serikali ya shilingi elfu sabini na tano kama shule za serikali zinavyofanya lakini hakuna shule binafsi inayofanya hivyo.                        
Aidha Mnyeti amefafanua  kuwa kodi zinazotakiwa kulipwa TRA na shule hizo ni kodi inayokatwa kwenye  mishahara ya watumishi waliojiriwa pamojana kodi ya mapato baada ya kupata faida ya biashara iliyofanyika.            
"Katika siku hamsini nilizotoa ni fursa ya mmiliki wa shule kwenda TRA kufahamu kiasi cha kodi anachodaiwa na kujipanga namna ya kulipa"  ameshauri Mkuu wa Wilaya huyo.    
Ingawa baadhi ya wamiliki wa shule hizo kulalamikia kutokupata faida katika uendeshaji wa shule zao lakni Mkuu wa wilaya alihoji mbona shule hizo hazifungwi kama hakuna faida.
"Haiwezekani kuendesha biashara miaka nenda rudi na useme haina faida bila kufunga biashara hiyo, wazazi wanalipa mamilioni ya mapesa hivyo ni lazima serikali ipate halali yake kupitia Kodi" alisisitiza zaidi Mnyeti            
Hata hivyo baadhi ya wamiliki wa shule hizo waliridhika na ulipaji wa kodi ya mapato na kukubaliana kwa pamoja kuridhika na muda huo waliopewa kukamilisha ulipaji wa kodi kama sheria inavyoelekeza.
 











Hivyo makala WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO

yaani makala yote WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wamiliki-wa-shule-binafsi-wasisitiziwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WASISITIZIWA KULIPA KODI YA MAPATO"

Post a Comment

Loading...