Loading...

WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO

Loading...
WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO
link : WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO

soma pia


WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO




Na Mtumwa Ally 
Mwambawahabari
MJUMBE wa Halmashaur Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Buguruni ,Barua Mwakilanga amesema ili kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho ni lazima kuwaondoa wasiliti wote wamechangia kukikosesha chama hicho kushika dola katika uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka 2015 katika kata mbali mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana amesema kuwa,ni jambo la kushangaza sana kuona mgombea ubunge anapata kura nyingi kuliko mgombea udiwani wa kata husika ,huu ni ukweli dhahiri huwa ndani ya chama kuna wasaliti wakubwa ambao wanakichafua chama kwa maslahi yao binafsi.

"Katika jimbo la Segerea tumepoteza madiwani wote 13 jambo ambalo limeonesha dhahiri kuwa kuna wasaliti wengi ndani ya chama chetu kutokana na kuwa haiwezekani mbunge kupata kura nyingi ndani ya kata kuliko muhusika mwenyew,"alisema Mwakilanga.

Aidha alisema,kutokana na hali hiyo ni vyema kwa viongozi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliotolewa na Mwenyeketi wa jumuiya ya wazazi (CCM )Taifa Abdalla Bulembo, kutaka kupelekewa majina yote ya wasaliti ndani ya chama na kumtaka Katibu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hata hivyo, alisema hana imani na viongozi ambao wamekabidhiwa kufatilia majina ya wasaliti hao kwani kuna taarifa hata hao viongozi wanashukiwa kuwa ni wasaliti hivyo hana uhakika kama wataweza kupeleka majina ambayo ni sahihi jambo ambalo limemtia wasi wasi mkubwa wa kuweza kufikia malengo ya kupata CCM mpya ambayo anaitaka Rais John Pombe Magufuli.

Aliongeza kuwa,Chama hizo kimekuwa katika harakati za uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya ndani ya chama ili kupata mabadiliko makubwa katika kuleta harakati za maendeleo kwa wananchi ili kufikia malengo hayo ni lazima kuwashughulikia ipasavyo wasaliti ndani ya chama.

Aliongeza kuwa,katika ziara iliyofanywa na Mwenyekiti huyo ilibainishwa kuwa viongozi ambao wamepewa nafasi za ukurugenzi wa kusimamia nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo shina ,matawi na kata ndio ambao wanashukiwa kukisaliti chama na kupelekea kupoteza nafasi mbali mbali ikiwemo udiwani.

"Endapo wasaliti wataachwa ndani ya chama na kuendelea kupanga safu zao kama wanavyopanga sasa hivi wameenda kutafuta makadi ya chama na kuwapa jamaa zao ili waweze kuja kuwachagua ,endapo hili litaachwa ile dhana ya Rais ya kuipata CCM mpya itakua ni ndoto"alisema Mwakilanga.


Hivyo makala WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO

yaani makala yote WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wasaliti-ndani-ya-chama-ni-kikwazo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WASALITI NDANI YA CHAMA NI KIKWAZO WASIFUMBIWE MACHO"

Post a Comment

Loading...