Loading...

WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS

Loading...
WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS
link : WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS

soma pia


WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS



Na Shamimu Nyaki-WHUSM.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea jumla ya shilingi 12,000,000 kutoka kwa Kampuni ya Multi Choice, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kuisaidia timu ya Serengeti Boys.


Dkt. Mwakyembe amezipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi cha fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali mwishoni mwa mwezi huu.



“Nawashukuru wadau wote wanaoendelea kuichangia timu yetu ya Serengeti Boys, leo nimepokea shilingi 10,000,000 kutoka Kampuni ya Mult Choice, shilingi 1,000,000 kutoka MISA TAN pamoja na shilingi 1,000,000 kutoka TAKUKURU”, alisema Dkt. Mwakyembe.



Ameongeza kuwa timu imeanza mashindano hayo vizuri japokuwa wametoka bila kufungana na timu ya Taifa ya Mali ambayo ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.



Aidha, ameahidi kuwa mchezo dhidi ya Timu ya Serengeti Boys na Timu ya Angola itakayochezwa Mei 18 mwaka huu itarushwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).



Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari amesema kuwa waandishi wa habari wameamua kuisaidia timu hiyo sio kwa kutumia kalamu zao kuwatangaza katika vyombo vya habari tu bali imeamua kuwasaidia kwa kuwachangia fedha.



“Tumeamua kuichangia timu yetu ili tuwape moyo zaidi wa kufanya vizuri kwani wameonesha jitihada katika mchezo wa mpira wa miguu,” alisema Bi. Salome. 


Hivyo makala WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS

yaani makala yote WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/waziri-mwakyembe-apokea-milioni-12_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS"

Post a Comment

Loading...