Loading...
title : CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA
link : CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA
CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.
Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Hamphrey Pole Pole, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais Dkt Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa.
Pole Pole amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi.
Pamoja na mambo mengine, Pole Pole, amesema kilichofanywa na Rais Magufuli ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini.
Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na MmIliki wa Kampuni ya Acacia kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa na Tanzania.
Hivyo makala CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA
yaani makala yote CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/ccm-yawataka-waliotajwa-katika-taarifa.html
0 Response to "CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA"
Post a Comment