Loading...
title : DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI
link : DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI
DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameiagiza Mamlaka ya mapato nchini TRA ngazi ya Wilaya ya Kinondoni kubadilisha mfumo wa ukusanyaji wa kodi ili kuongeza mapato ya serikali kutoka Bilioni 40 na kuendelea.
Hapi amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara la Wilaya ya Kinondoni katika hoteli ya Traventine Magomeni, amesema kuwa serikali ni lazima ikusanye kodi ambayo inatokana na wafanyabiashara.
Hapi amesema kuwa kufikia malengo ya zaidi ya ukusanyaji wa sh. bilioni 40 kwa kuwaingiza katika mfumo wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) kwa kuwa na vitambulisho maalum ili waweze kulipa kodi .
Amesema kuwa kuwaingiza machinga katika mfumo ndio utakuwa urasimishaji wa machinga hao kwa kuweza kukopesheka katika taasisi za fedha ikiwa ni pamoja kwa TRA kuweka vituo vya forodha katika Bandari Bubu za Mbweni ili kudhibiti mizigo inayoingia kinyemela kutokea visiwa Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya, Hapi Amesema kuwa kumekuwa na tatizo la uwepo wa leseni feki za biashara ambazo zinatolewa na watu feki nje ya ofisi za TRA na Manispaa ili waweze kukwepa kodi na kutafuta rekodi mpya ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakibuka kila siku katika Wilaya hiyo ambao wanastahili kulipa kodi kwa kuanza kupewa elimu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyabiashara Wilaya ya Kinondoni katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Traventine Magomeni.
Afisa Biashara wa Manispaa wa Manispaa ya Kinondoni, Mohamed Nyasama akizungumza juu ya hali ya biashara katika Manispaa hiyo .
Sehemu Wajumbe wa Baraza la Wafanyabiashara la Wilaya ya Kinondoni katika mkutano uliofanyika katika Hotel ya Traventine Magomeni leo jijini Dar es Salaam
Hivyo makala DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI
yaani makala yote DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/dc-hapi-aiagiza-tra-kinondoni-kuboresha.html
0 Response to "DC HAPI AIAGIZA TRA KINONDONI KUBORESHA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI"
Post a Comment