Loading...
title : EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA
link : EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA
EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA
Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara ndogondogo na saizi ya kati, yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika Nairobi, Kenya.
Tuzo za Banker za Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika wateja binafsi na biashara ndogo - Retail.
Akiongea kwa niaba ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka. Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 72 kwa mwaka 2016.”
Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA
yaani makala yote EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/exim-bank-tanzania-yapata-tuzo-ya-benki.html
0 Response to "EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA"
Post a Comment