Loading...

JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.

Loading...
JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.
link : JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.

soma pia


JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.


Related image

Na Tiganya Vincent
RS-TABORA
20.6.2017

Mahakama ya Tanzania imesema itaendelea kuboresha Mahakama za Mwanzo zilizopo na kujenga mpya walau katika kila Kata kwa ajili ya kuhakikisha kuwa huduma za usikilizaji wa mashauri mbalimbali zinafanyika karibu na wananchi  na hivyo kutoa fursa kwao kuendelea na shughuli nyingine za kimaendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo(jana) mjini Tabora na Jaji Kiongozi  Mhe. Ferdinand Wambali wakati wa ziara ya kikazi katika mikoa ya Tabora na Kigoma kwa ajili ya kukagua shughuli za usikilizaji wa mashauri mbalimbali kama walivyojiwekea malengo ya kuharakisha.

Jaji Kiongozi alisema kuwa kuna Wilaya zinategemea Mahakama za maeneo mengine na nyingine kama vile Sikonge ina Mahakama moja tu jambo ambalo linawafanya wakazi wake wakati mwingine kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za Kimahakama katika Wilaya ya Tabora.

Alisema kuwa Mahakama ya Tanzania itaendelea kuboresha Mahakama za Mwanzo zilizopo na kujenga mpya katika maeneo yote ambayo hayana huduma hiyo kulingana na upatikanaji wa fedha ili kuhakikisha kuwa huduma hizo wananchi wanazipata karibu na wanapoishi kwa ajili ya kutumia muda mfupi kufuatilia mashauri na uliobaki katika shughuli nyingine za kiuchumi.

Jaji Kiongozi huyo aliongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kila shauri linalofika katika Mahakama ya Mwanzo lisizidi miezi sita na lile linakwenda katika Mahakama za Wilaya na zile za Hakimu Mkazi lisizidi mwaka mmoja na Mahakama Kuu miaka miwili.

Alitoa wito kwa Mamlaka zinazohusika na utoaji wa ardhi kutoa kipaumbele pindi Mahakama inapohitaji eneo la ujenzi majengo ya Mahakama ili kazi ifanyike kwa wakati na hivyo wananchi waweze kusafiri umbali mfupi kufuata huduma za kutafuta haki yao.

Jaji Kiongozi alisisitiza kuwa ucheleweshaji unaoweza kufanyika wakati wao wanahitaji eneo la ujenzi linawaathiri pia wananchi wanaokuwa wakihitaji huduma hiyo kwa karibu zaidi.

Katika hatua nyingine Jaji Kiongozi Wambali alisema kuwa Mahakama imo katika mpango wa kuhakikisha Mashauri yalichukua muda mrefu yanamalizika haraka sana ili kutoa fursa kwa wahusika kuendelea na shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kuendelea na kesi.

Alisema kuwa hatua hiyo ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya Mahakama ili iweze kurahisisha utendaji wa shughuli za chombo hicho.


Hivyo makala JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.

yaani makala yote JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/jaji-kiongozi-tutaendelea-kujenga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JAJI KIONGOZI-TUTAENDELEA KUJENGA MAHAKAMA ZA MWANZO ILI KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI."

Post a Comment

Loading...