Loading...
title : Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali
link : Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali
Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali
Immaculate Makilika- MAELEZO
mwambawahabari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema Kampuni ya madini ya Barrick imekuabali kufanya mazungumzo na Serikali ikiwa ni pamoja na kulipa fedha ambazo Serikali inadai kwa kufanya shughuli zake hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation inayomiliki kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton leo Ikulu jijini Dar es Salaama, Rais Magufuli amesema kampuni ya Barrick imekubali mazungumzo na Serikali ya Tanzania na kulipa fedha wanazodaiwa.
“Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ilikufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisema kuwa licha ya kampuni hiyo kukubali kulipa fedha wanazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu hapa nchini.
Naye, Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo inatakiwa kulipa kwa Serikali ya Tanzania.
Mazungumzo hayo kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Ian Myles na Waziri wa Katiba na sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Hivyo makala Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali
yaani makala yote Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/kampuni-ya-barrick-yakubali-kulipa-deni.html
0 Response to "Kampuni ya Barrick yakubali kulipa deni lake kwa Serikali"
Post a Comment