Loading...

KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI.

Loading...
KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI.
link : KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI.

soma pia


KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka viongozi na watumishi wote nchini kuzingatia nidhamu kama msingi wao wa utendaji kazi pamoja na kanuni na maadili ya utumishi wa umma ili utumishi wao uweze kuwa mzuri.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo alipokutana na watumishi Mkoani Singida na kusikiliza matatizo, kero, changamoto pamoja na kupata maoni ya namna ya kuboresha utumishi wa umma kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma nchini.

Amesema kila mtumishi anapaswa kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu ya hali huku akiwasisitiza viongozi hasa wa watumishi wa umma kuwasikiliza watumishi wao pale wanapotoa maoni yao bila kuyapuuzia au kuwakatisha tamaa kwa vitisho.

“Ukiwa kiongozi unapaswa uweze kuishi na kila aina ya mtu, kuna watumishi wengine hawawezi kufichaficha mambo ukikosea wanakusema bila kupepesa maneno, wengine ni waoga hawawezi kukueleza wazi ila wanatumia mbinu mbali mbali, ukiwa kama kiongozi uwe tayari kupokea ushauri ili uweze kuboresha utendaji wako”, amesisitiza Dkt Ndumbaro.

Dkt Ndumbaro amewaasa viongozi hao kuwapongeza watumishi wanaofanya kazi kwa bidii na wenye nidhamu ili iwe motisha kwa wale wavivu huku akiwataka kuwachukulia hatua wale wazembe na ambao hawataki kufuata kanuni na maadili ya utumishi wa umma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani) kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
 Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro alipowatembelea katika kuadhimisha wiki ya utumishi umma.
 Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida Mwalimu Eva Mosha akitoa maoni yake kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro aliwapotembelea watumishi wa Mkoa wa Singida katika kuadhimisha wiki ya Utumshi wa Umma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI.

yaani makala yote KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/katibu-mkuu-utumishi-asisitiza-nidhamu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KATIBU MKUU UTUMISHI ASISITIZA NIDHAMU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI."

Post a Comment

Loading...